MOTO WATEKETEZA MADUKA KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Apr-13/17:09:19 Moto mkubwa umezuka katika eneo la mtaa wa Soga katika halmashauri ya mji na kutekeza duka la vifaa vya baiskeli na pikipiki, duka la vifaa vya kielektroniki na sehemu ya kukatia nywele na kusababisha hasara ya fedha na mali ya fedha na mali. Wananchi kwa kushirikiana gari la kuzima moto la halmashauri ya mji wa Kibaha walifanya kazi bega kwa bega kuhakikisha moto huo hauleti madhara zaidi kwa nyumba zilizopo jirani ya eneo la tukio ambalo lilisababisha mmiliki wa duka la vifaa vya baiskeli na pikipiki aliyejulikana kwa jina la DEO kutokomea kusikojulikana. Lakini taarifa nyingine zinasema baadhi ya watu baadaya kumuona alivyokuwa amechanganyikiwa waliamua kumtuliza na kumpeleka kwa kaka yake kwa ajili ya kuliwazwa kufuatia janga hilo ambalo limemwacha akiwa hana nyuma wala mbele kibiashara ingawa bado kuna matumaini kimaisha. Naye shuhuda wa tukio hilo Bw. IBRAHIM CHAKA amesema wao walianza kuona moshi ukifuka katika duka la vifaa vya Baiskeli na pikipiki na muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndivyo moto huo ulivyokuwa unazidi kuwa mkubwa huku baadhi ya wanajamii wakichukua hatua ya kupiga simu kwa kikosi cha kuzima moto halmashauri ya mji wa Kibaha ambao walifika katika eneo katika kipindi mwafaka. Mmiliki wa nyumba hiyo aliyejulikana kwa jina moja la FUNDI MUSSA kwa upande wake yeye alikuwa analia na baadhi ya watu waliojitokeza kutoa msaaada katika tukio hilo kutumia mwanya huo kumwibia baadhi ya vifaa vyake kama meza, deki ya cd na vifaa vingine kiasi cha kuanza kuwakamata baadhi ya watu akiwahusisha na wizi huo. Naye Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Soga BW. ALLY MGAYA amesema yeye binafsi ameshuhudia moto huo na amepongeza ushirikiano ulioonyeshwa na wananchi katika kukabiliana na hali hiyo ambayo ingeachiwa hivi hivi ingeweza kusababisha madhara zaidi kwa nyumba ambazo zipo karibu na eneo la tukio. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA