WANANCHI WAGOMEA BARAZA LA MADIWANI KIBAHA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/04/25/18:04:09
Katika hali inayoaashiria kukosekana kwa ushirikishwaji kwa wananchi kuhusiana na ratiba ya vikao vya Baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha kumesababisha kukosa ushiriki wa wananchi kutokana na kutokuwepo na taarifa za mapema za vikoa hivyo na wakati mwingine baadhi ya watendaji kukalia taarifa ambazo zinapaswa kufikishwa kwa wananchi.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia viti ambavyo vilipaswa kukaliwa na wananchi vikiwa wazi na ukumbi huo kujazwa na madiwani na wakuu wa idara pekee na hivyo kufanya kikao hicho kupoteza mvuto wake wa kawaida ambao ulikuwa na lengo la kupanua demokrasia katika ngazi ya serikali za mitaa.
Kutokana na hali hiyo ilimbidi wa Chama Cha Mapinduzi halmashauri ya wilaya ya Kibaha BW. HAMIS KANESA kuchukua fursa hiyo kuwataka watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanaboresha utoaji taarifa kuhusiana na ufanyikaji wa vikao hivyo kama ratiba inavyoainisha.
Mbali ya kujitokeza hali hiyo Madiwani na watendaji hao wa halmashauri walipata fursa ya kupewa semina fupi kuhusiana na sheria namba 13 ya 1995 ya maadili ya viongozi wa umma, Ambapo Afisa wa maadili ya BI.LILIAN AKITANDA kutoka sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma amesema maadili ya sekretarieti ya umma itajaribu kadri iwezavyo kujenga na kufuata msingi ambao utafuatilia mienendo ya viongozi wa umma.
BI. AKITANDA amebainisha kuwa viongozi wa umma wanatakiwa kufanya maamuzi katika utekelezaji wa kila siku wa majukumu yao na kutoa maamuzi kwa kufuata misingi ya haki na kwa mujibu wa sheria, kwa maslahi ya umma na kulingana hali ya kila jambo ili kuimarisha uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma.
END.
Comments
Post a Comment