TALAWANDA YAZITOA HOFU TAASISI ZA MOKOPO
Na Omary Mngindo, Bagamoyo
Juni 29
SERIKALI Kata ya Talawanda wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imezitoa
hofu taasisi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kwamba itawasimamia
ipasavyo wakazi ndani ya Kat hiyo watakaoomba mikopo ili kuhakikisha
wanairejesha kwa wakati.
Diwani wa Kata hiyo Bw. Said Zikatimu ameyasema hayo juzi akifungua
mafunzo ya siku moja kwa wajasiriamali wapatao 293 kupitia vikundi 58
ndani ya Kata yaliyoendeshwa na taasisi ya TAGIDOyenye makazi yake
wilayani humo inayojihusisha na utoaji wa elimu hiyo ikishirikiana na
tasisi za kifedha lengo kuviinua vikundi mbalimbali.
"Niwahakikishie kwamba serikali ya Kata itashirikiana na bega kwa bega
na viongozi wake ngazi mbalimbali ili kuhakikisha vikundi vyote
vitakavyokopa tunavisimamia ipasavyo na hatimaye mikopo inarejeshwa
kwa wakati hivyo niwaondoe hofu juu hilo," alisema Zikatimu.
Aliongeza kuwa katika vikundi hivyo vyote vimesajiliwa na vina hati
kutoka kwa msajili mwenye dhamana na kwa sasa vinaendelea na mipango
ya ufunguaji wa akaunti kwenye benki na kwamba wakati wowote vitaanza
kufuatilia taratibu za kukopa fedha ili vijiendeshe kama
vilivodhamiria.
Kwa upande ofisa kutoka TAGIDO Bw. Hamza Mfaume amesema kuwa ofisi
hiyo inajihusisha na utoaji wa elimu ya ujasiriamali lengo kutambua
fursa yao katika kuomb amikopo kwenye benki ili wajiekwamue kiuchumi
kupiti vikundi na mtu binafsi.
"TAGIDO inajikita zaidi katika utoaji wa elimu ya ujasiriamali kwa
watu kupitia vikundi mbalimbali ambapo lengo letu kuu i kuhakiisha
walengwa hao wanatumia fursa ya kukopa fedha kwenye taasisi za kifedha
na hatimaye wanajikwamua kiuchumi kupitia fursa hiyo," alisema Bw.
Hamza.
Naye mmoja wa maofisa kutoka benki ya NMB Bw. Mark Andulu alisema kuwa
kwa sasa benki hiyo imejikita zaidi maeneo ya vijijini kwa lengo la
kuwapatia elimu na fursa wakazi kunufaika na huduma bora ambayo
inaendelea kutolewa na benki hiyo.
"Uongozi wa benki Makao Makuu kwa sasa umeamua kuelekeza nguvu zaidi
maeneo ya pembezoni mwa mji lengo kuhakikisha inawafikia wananchi
ambao badhi yao hawana elimu juu ya huduma bora inayotolewa na benki
yetu, hivyo nitumie nafasi hii kuwajulisha kwamba benki yenu
imeanzisha huduma nyingine ya haraka inayoitwa chapchap akaunti,"
alisema Andulu.
MWISHO.
Comments
Post a Comment