WANANCHI WAIGOMEA TANROADS
Ben Komba/Pwani-Tanzania/Sunday, June 01, 2014
Wakazi wa Kata ya Pangani na
Kata ya Maili moja halmashauri ya mji wa Kibaha wamewazuia wakala wa
barabara Tanzania TANROADS kuweka mawe katika maeneo yao kabla
hawajalipwa fidia stahili kutokana maeneo yao kummegwa kutokana na
upanuzi wa barabara ya TAMCO-MAPINGA.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi, Diwani wa Kata ya MAILIMOJA BW.ANDREW LUGANO akiaambatana
na mwenyekiti wa serikali ya machinjioni,amesema inashangaza kuona
TANROADS wanaweka mawe kana kwamba wameshakamilisha taratibu za kulipa
fidia.
BW.LUGANO amebainisha kuwa
tahtimini katika eneo hilo imeshafanyika na kinachosubiriwa na kwa
TANROADS kulipa fidia kwa wananchi hao, toka kwa sasa wanashindwa
kuyaendeleza kuhofia kuvunjwa na TANROADS na hivyo kuwafanya kuishi
katika hali ya wasiwasi na kushindwa kujua hatima yao.
BW.LUGANO ameshangazwa na
hatua hiyo ya TANROADS kuanza kuweka mawe kabla ya kulipa fidia kwa
wananchi, kitu ambacho hakikubaliki hata kidogo kwa wananchi ambao
maeneo yao yanapitiwa na barabara hiyo.
Akizungumzia suala hilo Meneja
wa TANROADS Mkoa wa Pwani, BW.TUMAINI SARAKIKYA ameelezea kuelewa kwake
juu ya mgogoro wa wananchi kuhusiana na madai ya fidia yao, ana
amemweleza mwandishi wa habari hizi kuwa suala lao linashughulikiwa na
litafanyiwa kazi muda wowte kuanzia sasa.
END.
Comments
Post a Comment