UZINDUZI WA VITAMBULISHO VYA URAIA WAFANYIKA PWANI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/30/6/2014
Mkuu wa mkoa wa Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA amepongezea
hatua ya serikali ya kutoa vitambulisho vya uraia ili kuweza kutambua wageni na
raia halali wa nchi hii ya Tanzania.
Akizungumza katika kipindi cha uzinduzi wa usajili wa
watu mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amesema jukumu hilo linaloratibiwa na NIDA ni
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi na ni maelekezo ya
serikali ya awamu ya nne.
Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amewasisitiza
wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha jukumu hilo linatekelezeka kama
serikali ilivyoaagiza, kwa kuipa NIDA ushirikiano wa hali na mali ikiwa pamoja
na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa vitambulisho vya uraia.
Ameagiza iwapo kutakuwa na tatizo lolote amewataka
watendaji kumpa taarifa katika kipindi mwafaka, ili kuepuka kukwamisha zoezi
hilo muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa letu.
Awali akizungumza kukmaribisha Mkuu wa mkoa wa
Pwani,Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa, BW.DICKSON MAIMU amebainisha
kuwa mfumo wa utambuzi na usajili wa watu umeleta mabadiliko makubwa ya
kiuchumi na kijamii katika serikali nyingi duniani ambazo zimejenga mfumo huo.
BW.MAIMU amebainisha dhana kuu ya mfumo huu ni kujibu
maswali makubwa ambayo nani ni nani?, yuko wapi na anamiliki nini na anafanya
nini, majibu yakipatikana yatatoa fursa nyingi na kuongeza tija katika utendaji
wa taasisi za umma na binafsi, kwa kurahisisha suala la utambuzi wa watu na
kuweza kutroa huduma kwa urahisi zaidi.
BW.MAIMU amesisitiza kuwa mfumo huo utakuwa na faida
nyingi kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni,katika utekelezaji wa mradi huu, mamlaka
itatoa vitambulisho katika makundi matatu kwa maana ya Watanzania wazawa,
wageni wakaazi na wakimbizi.
END.
Comments
Post a Comment