WLAC YAWAPATIA WASAIDIZI WA KISHERIA MAFUNZO
Ben Komba/Pwani-Tanzania/
Kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake-WLAC- kimetoa mafunzo kwa wasaidiz wa kisheria
wilayani Kibaha ili kuweza kuwajengea uwezo na kuwawezesha kusaidia jamii
katika maeneo yao wanaokabiliwa na migogoro mbalimbali.
Afisa mradi msaidizi wilaya ya Kibaha, kutoka WLAC ambao
wanasaidiwa kwa ufadhili wa LEGAL SERVICES FACILITIES, BI.SABRINA MTEGA
amebainisha kuwa mradi huo umelenga kutoa mafunzo ya siku 25 kwa wasaaidizi wa kisheria wilayani Kibaha.
BI.MTEGA ameongeza kuwa anatarajia mara baada ya kukamilika
kwa awamu ya tatu nay a mafunzo hayo, wasaidizi wa kisheria watakuwa
wamefundishwa mbinu mbali mbali za kupambana na changamoto za kisheria ikiwa
pamoja na kutoa rufaa klwa masuala ambyo yanahitaji utaalamu zaidi wa kisheria,
BI,MTEGA amewataka wasaidizi wa kisheria wanaopatiwa mafunzo
wafanye kazi kwa mshikamno na kuweka ubinafsi pembeni ili malengo ya mradi
yaweze kufikiwa.
Naye mwezeshaji kutoka WLAC,BW.ROBERT CHUWA akitoa mada ya
haki za binadamu mbele ya washiriki wa mafunzo hayo esema kuwa haki za binadamu
ni stahiki aambayo binadamu anazaliwa
nayo na wala si hisani.
BW.CHUWA amefafanua kuwa nchini Tanzania
haki za binadamu ziliingizwa rasmi katika katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya
mwaka 1984 ilipofanyiwa marekebisho, na kujitokeza vizazi mbalimbali vya haki
za binadamu.
END
Comments
Post a Comment