MKUU WA MKOA WA PWANI AZINDUA VIATAMBULISHO VYA URAIA.

 
Ben Komba/Pwani-Tanzania/30/6/2014
Mkuu wa mkoa wa Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA amepongezea hatua ya serikali ya kutoa vitambulisho vya uraia ili kuweza kutambua wageni na raia halali wa nchi hii ya Tanzania.
 
Akizungumza katika kipindi cha uzinduzi wa usajili wa watu mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amesema jukumu hilo linaloratibiwa na NIDA ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi na ni maelekezo ya serikali ya awamu ya nne.
 
Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani, BI.MAHIZA amewasisitiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha jukumu hilo linatekelezeka kama serikali ilivyoaagiza, kwa kuipa NIDA ushirikiano wa hali na mali ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa vitambulisho vya uraia.
 
Ameagiza iwapo kutakuwa na tatizo lolote amewataka watendaji kumpa taarifa katika kipindi mwafaka, ili kuepuka kukwamisha zoezi hilo muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa letu.
 
Awali akizungumza kukmaribisha Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa, BW.DICKSON MAIMU amebainisha kuwa mfumo wa utambuzi na usajili wa watu umeleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii katika serikali nyingi duniani ambazo zimejenga mfumo huo.
 
BW.MAIMU amebainisha dhana kuu ya mfumo huu ni kujibu maswali makubwa ambayo nani ni nani?, yuko wapi na anamiliki nini na anafanya nini, majibu yakipatikana yatatoa fursa nyingi na kuongeza tija katika utendaji wa taasisi za umma na binafsi, kwa kurahisisha suala la utambuzi wa watu na kuweza kutroa huduma kwa urahisi zaidi.
BW.MAIMU amesisitiza kuwa mfumo huo utakuwa na faida nyingi kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni,katika utekelezaji wa mradi huu, mamlaka itatoa vitambulisho katika makundi matatu kwa maana ya Watanzania wazawa, wageni wakaazi na wakimbizi.
 
END.
--

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA