VIFO VYA KINAMAMA NA WATOTO VYAPUNGUA PWANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/Tuesday, August 26, 2014
Kituo cha
afya Kibiti wilayani Rufiji mkoa wa Pwani kimefanikiwa kwakiasi kikubwa
kupunguza vifo vya kinamama na watoto wakati wa kujifungua na baada ya
kujifungua.
Daktari
msaidizi wa kituo hicho,BW.DKT CHAGI LYIMO amesema hayo alipokutana na
waandishi wa habari 18 waliotembelea kituo hicho kutoka Dar es Saalam,Pwani na
Morogoro ambapo wanapatiwa mafunzo juu
masuala ya afya ya uzazi na jinsia yaliondaliwa na shirika lisilo la kiserikali
la WORLD LUNG FOUNDATION.
Amefariki
kutokana na matatizo ya uzazi,mafanikio hayo yametokana na usaidizi wanaopata
kutoka WORLD LUNG FOUNDATION ambao wamewasaidia kwa njia moja au nyingine
katika kuhakikisha wanapunguza vifo vya mama na mtoto.
Bw.LYIMO
amebainisha juhudi ambazo WORLD LUNG FOUNDATION, ni pamoja na kujengewa wodi ya
uzazi,chumba cha upasuaji nakupatiwa gari la kubeba wagonjwa.
Naye Mkunga
wa kituo hicho,BI.DARIA NDUNGURU amefafanua kuwa yeye kwa nafasi yake
ameshuhudia kupungua kwa asilimia kubwa inayotolewa na WLF katika kuwapatia
nyenzo za kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama.
Akizungumzia
juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao
ya kila siku, BI.NDUNGUR amesema upungufu wa damu ndio tatizo kubwa hasa
inapohitajika mama mjamzito anahitajika kufanyiwa upasuaji.
END.
Comments
Post a Comment