FIVE STAR MODERN TAARAB YATISHA KIBAHA



Ben Komba/Pwani-Tanzania/

Kundi la muziki wa taarab la Five Star limeiteka mamlaka ya Mji mdogo wa Mlandizi baada ya kukaa kimya kwa kipindi Fulani kufutia ajali iliyoua wanamuziki wao 13.

Kiongozi wa kundi hilo, BW.ALLY JUMA amesema pembeni ya ukumbi wa CONTAINER BAR Mlandizi kuwa wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo ya Taarab kuwaunga mkono na kutosikiliza maneno ya watu wasiowatakia mema bendi hiyo.

Ameshauri vikundi vya muziki wa taarabu kujitokeza na kuunda umoja ambao utaangalia maslahi yao na kulinda haki zao, kutokana watu wengi kuiba kazi za wasaanii na kuwanyima mapato kutokana na wizi huo.

Nye Mkurugenzi wa ukumbi huo wa CONTAINER BAR Mlandizi,BW.FRANK MWALEMBWE ameelezea nia yake ya kuhakikisha kuwa kunakuwepo na burudani kila miwsho wa wiki katika ukumbi huo ili kutoa fursa kwa wasanii wa Tanzania kuonyesha uwezo wao.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA