RAIS MAGUFULI AMWAGIWA SIFA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/27/05/2017 09:44:00
Rais JOHN
POMBE MAGUFULI amepongezwa kufuatia hatua mbalimbali anazochukua kukabiliana na upotevu wa fedha za mchanga wa
madini ambao uliokuwa unaigharimu nchi zaidi ya matrilioni ya shilingi zilizokuwa zinapotea kwenye
baadhi ya mikono ya watumishi wa serikali wasio waaminifu.
Mkurugenzi mtendaji
wa shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE la mjini
Kibaha, BW.ISRAEL ILUNDE ameyasema hayo wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hizi pembeni mwa jukwaa la ufahamu wa
kiraia linalofanyika kila ya ijumaa ya
mwisho wa mwezi.
Ambapo amesema
hatua ambazo amekuwa akizichukua kudhibiti uvujaji wa mapato mbalimbali hazina
budi kuungwa mkono na umma wa Watanzania kwani zitawezesha nchi kuelekea katika
maendeleo endelevu kwa ustawi wa n chi katika utoaji wa huduma mbalimbali za
kijamii.
Bw. ILUNDE
ameongeza kitendo chake cha kutofumbia macho vitendo hivyo ni ishhara tosha ya
kuonyesha lengo lake la kutaka kuikwamua nchi kutoka katika umaskini na kufikia maendeleo yanayohhitajika ili
kuleta mustakabali mwema wan chi yetu.
Akitoa mfano
wa hivi karibuni ya kubaini matrilioni ya fedha ambazo zilikuwa zinapotea
kutokana na usafirishaji wa mchanga wa madini uliokuwa unaigharimu serikali zaidi ya shilingi
Trilioni moja za Kitanzania kila mwezi, na kuikosesha serikali mapato katika
kipindi cha takribani miaka 20.
Mmoja ya
wananchi waliohudhuria Jukwaa hilo la ufahamu wa kiraia , BI
ANASTAZIA CHARLES amesema kuwa wakati sasa umefika kwa fedha ambazo zimekuwa
zinaokolewa na juhudi za Rais JOHN MAGUFULI katika kubana uvujaji wa mapato ya
serikali kuelekezwa katika uimarishaji huduma za kijamii katika kuboresha upatikanaji wa madawa mahospitalini, ujenzi wa
miundombinu ya barabara za vijijini na kuboresha mazingira ya utendaji katika
sekta ya elimu na maeneo mengineyo.
END
Comments
Post a Comment