SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LALAMIKIWA URASIMU MALIPO YA WAKANDARASI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/04/05/2017 09:53:24
Baadhi ya
wazabuni wanaofanya kazi na Shirika la Elimu Kibaha wamelalamikia kitengo cha
ukaguzi kwa kuwakata fedha ambazo wamepatana kulipwa kwa zabuni wanapewa kwa
visingizio ambavyo havina mantiki.
Uchunguzi ambao
umefanywa na mwandishi wa habari hizi kwa takribani wiki mbili kufuatia
malalamiko ya mmoja wa wazabuni ambaye alipatiwa kazi ya kufanya matengenezo
katika chumba cha kuzalishia dripu za kwa ajili ya wagonjwa, BW.KABUGI MNDEME
na baadaye kulipwa nusu ya fedha iliyopo katika makubaliano.
BW.MNDEME
amesema kuwa yeye aliingia makubaliano ya kuweka milango na madirisha ya aluminium katika chumba hicho cha
kuzalisha dripu za maji ya kuongezewa wagonjwa kupitia LPO No. 20161163 ambapo
kwa upande wake ametimiza wajibu na kukamilisha
matengenezo hayo ambayo gharama yake halisi ilikuwa shilingi
5,892,500.00.
BW.MNDEME
ameongeza kuwa cha kushangaza mara kazi ilipokamilika ndipo urasimu wa malipo
ulipoanza, kukaanza kuzuka sababu mbalimbali ikiwa pamoja na kuainisha maeneo
yenye kasoro ambayo mkandarasi alirudia kazi ile kama maelekezo yalivyotolewa
na Afisa kutoka idara ya ukaguzi, BW. FRED KAMBI, wasiwasi wake mkubwa ni
kwamba malipo hayo yamefanywa kupitia LPO ambayo tayari ilishapita katika mfumo
wa malipo ya serikali.
Lakini haikutosha
kumpatia haki yake na matokeo yake kukaandikwa barua nyingine tofauti na LPO ya
awali ambayo ikadaiwa kuwa mzabuni hastahili kulipwa fedha iliyoainishwa awali
na kuamua alipwe shilingi milioni
3,282,200.00 (milioni tatu laki
2themanini na mbili elfu na mia mbili), Kitu ambacho hakukubaliana nacho.
BW.KABUGI
amefafanua kuwa changamoto kubwa ambayo wazabuni wamekuwa wakikumbana nacho ni
kwa mmoja wa wakaguzi hao kuwa na kampuni yake, ambayo imeshafanya kazi katika jengo
lililokuwa chumba cha upasuaji na kujilipa shilingi Milioni 26 ambapo ukaguzi
ulifanywa na afisa msaidizi wa kitengo cha ukaguzi cha Shirika hilo ilihali
malipo hayalingani na kazi ambayo imefanyka ya ukarabati, na hivcyo kutumia
nafasi hiyo kuwachosha wazabuni wan je ili kazi zote zichukuliwe na kampuni
hiyo.
Juhudi za
kumpata Afisa wa ukaguzi wa shirika la elimu Kibaha, BW.FRED KAMBI ziligongwa
mwamba kwa kumtaka mwandishi wa habari hizi kuonana kwanza na msemaji wa
Shirika, BI.LUCY SEMINDU ambaye kwa upande wake alifanya jitihada kubwa na kuweza
kuonana na Kaimu Mkurugenzi BW.ROBERT SHILINGI.
Kaimu Mkurugenzi
wa Shirika la Elimu Kibaha, BW.ROBERT SHILINGI alimwambia mwandishi wa habari
hizi kuwa jambo hilo lipo ndani ya uwezo wa Shirika na kuahidi kulishughulikia
kikamilifu na kumtaka mkandarasi huyo kufika ofisini kwake ili waweze
kulizungumza kwa lengo la kulitatua.
Hata hivyo
baada ya kukutana mkandarasi na uongozi wa shirika la elimu Kibaha iliamriwa
kuwa wao msimamo wao upo vilevile na kumtaka mkandarasi huyo kuchukua hatua
nyingine iwapo hakuridhika na maamuzi hayo.
INSERT:ROBERT
SHILINGI
END
Comments
Post a Comment