MBUNGE AHIMIZA UPENDO NA UMOJA CCM.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-Dec-12/17:03:00
Mbunge wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SYLVESTER KOKA amewataka wanaCCM MJINI Kibaha mjini kutoogopa kuwakosoa viongozi wake moja kwa moja badala ya kusemea pembeni na kutoa fursa kwa maadui kukidhoofisha chama chao.
Ameyasema hayo akiwa katika ziara maalum ya kuimarisha uhai wa chama mjini Kibaha katika kata ya Mailimoja Tawi la TAMCO, BW. KOKA amesema tabia ya baadhi ya wana CCM kutotumia nafasi yao kama wanachama wa chama hicho kuongea na viongozi juu ya mambo mbalimbali ambayo wanayafahamu na badala yake kwenda kuongea mahali ambapo hapastahili ndio zinazokichimbia karibu chama hicho.
BW. KOKA ametoa mfano wa kuwa haiwezekani Mzazi akaenda kumsifia mwanaye kama labda analala nje kwa jirani yake badala ya kujadili suala lile na mwanae, kwani kwa kumueleza vile jirani hakutasaidia kurekebisha hali ya mambo badala yake inaweza kusababisha mambo kuharibika zaidi.
Mbunge huyo wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SYLVESTER KOKA ameongeza kuwa kipindi hiki ni cha mageuzi ya ndani ya chama, ambapo utamaduni wa kukosoa na kukosolewa unachukua nafasi kubwa katika kukijenga chama na kutotoa nafasi wa maadui kujiingiza katika masuala ya uendeshaji wa chama, na kutokana na hilo tabia ya kusengenyana nje ya vikao vya chama iachwe mara moja na kama kuna tatizo lolote juu yake basi mtu asisiste kuwasiliana naye.
Katika ziara hiyo Mbunge huyo ya kutembelea matawi na mashina ya chama cha mapinduzi amekuwa akikutana na vilio mbalimbali vya wananchi kama ilivyojidhihirisha katika mkutano wake wa Tawi la Yombayomba, Kata ya Mailimoja ambapo ilimlazimu kumchangia mjane mmoja ambaye nyumba yake imeanguka kufuatia mvua kali zilizonyesha juzi, katika baadhi ya maeneo amekuwa akitoa misaada mbalimbali ikiwa kutimiza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni.
END.
Comments
Post a Comment