WAZAZI WATAKA KURUDISHIWA MALI ZAO.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/25-Dec-12/22:57:12
Wanachama wa wa Jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi mjini Kibaha wamemtaka mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kuirudisha shule ya wazazi ya Sekondaro Kaole iliyopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani kurudishwa kwa mikononi mwa Jumuiya hiyo.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Jumuiya ya wazazi kata ya Kongowe mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya jumuiya hiyo kata ya Kongowe, DR. NASSORO KAZAMBO ameitaka serikali ya chama cha mapinduzi kurudisha shule hiyo kwa jumuiya ya wazazi ili kutoa fursa kwa jumiya hiyo kuingia ubia na mashirika mbalimbali ili kuziendesha shule hizo.
DR. KAZAMBO amesema kitendo cha kupora mali za jumuiya ya wazazi na baadaye kubezwa kuwa ni jumuiya ambayo haitoshi hilo halikubaliki na hasa ikizingatiwa kuwa jumuiya hiyo ni tajiri na kinachosokana ni usimamizi wa mali hizo na kwa kuingia ubia na watu mbalimbali katika kuzisimamia na kuziendesha.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mjini Kibaha, DR. ATHUMAN ZAHORO MOKIWA amesema kuwa suala hilo atalichukua ili likapatiwe ufafanuzi sahihi ili kurejesha mali za jumuiya hiyo.
Aidha DR. MOKIWA amewataka wanachama wa Jumuiya ambayo inaingia katika kila Jumuiya ya chama hicho kuanzia Vijana na wanawake, toka mtu yoyote mwenye umri wa miaka 18 tayari anakuwa na sifa ya kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo, kuwa wabunifu ili kuwezesha jumuiya hiyo kujitegemea badala ya kubaki kuwa ombaomba.
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi mjini Kibaha, DR. MOKIWA amewataka jumuiya ya wazazi kufungua akaunti na kutafuta maeneo kwa ajili ya kujenga ofisi za jumuiya ambayo kwa sasa imekuwa ikidandia ofisi za jumuiya nyingine hali ambayo inaifanya kushindwa kufanaya kazi kwa ufanisi.
END.
Comments
Post a Comment