KANSA YA SHINGO YA KIZAZI TISHIO.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-Dec-12/00:45:48
Imesemekana mjini Kibaha kumekuwepo na tatizo kubwa la kansa ya shingo ya uzazi, ambapo katika kila mwaka watu 500,000 wanaogundulika kuwa na kansa ya shingo ya uzazi 275000 wanakufa kila mwaka.
Msimamizi wa Kitengo cha kansa ya shingo ya uzazi kituo cha afya mkoani mjini Kibaha, BI. JULIETH SANGA amesema tatizo hilo kwa sasa ni kubwa kwa kiwango cha asilimia 50.9/100,000 na vifo vinavyosababishwa navyo ni wastani 37.5/100,000.
BIBI.SANGA amebainisha kuwa kutokana na takwimu hizo ugonjwa huo umekuwa tishio kwa kinamama na mzigo kwa wanaougua na wanaouguza kwani Tanzania imekuwa iko juu kulinganisha na nchi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla wake.
BIBI. SANGA amefafanua chanzo cha ugonjwa huo ni kuanza mapenzi katika umri mdogo na hasa wanapokutana na mwanaume mwenye virus vya PAPPILOMA wanaoishi katika mwili wa mwanaume bila kumletea madhara.
Amesisitiza hatari ya maambukizi inazidi kwa mwanamke kuwa na wapenzi wengi, magonjwa ya zinaa, kuvuta sigara, HIV na upungufu wa kinga mwilini na wakati mwingine kurithi.
BIBI. JULIETH SANGA Msimamizi huyo wa kitengo cha kansa ya shingo ya uzazi, ameongeza kuwa kansa hiyo inaweza kukingika iwapo itaguinduliwa ikiwa katika hatua ya awali, kuchelewa kufanya mapenzi, matumizi ya kondom na kujali afya kwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara.
END.
Comments
Post a Comment