BENKI YA VIJANA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-Dec-12/09:58:38
Vijana mjini Kibaha watafaidika kutokana na hatua ya kuanzishwa benkia ya vijana ambayo itkuwa inajishughulisha na kuwawezesha vijana kwa kuwapatia uwezeshaji wa hali na maki katika kuwasaidia kujikwamua nahali ngumu ya maisha inayowakabili kada hiyo katika jamii.
Mratibu wa Benki ya vijana wilayani Kibaha, BI. LULU MKOMAMBO amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa makusudi katika kumwezesha kijana kujikwamua na hali duni aliyonayo, na hasa ikizingatiwa vijana ndio kundi kubwa ambao wanakadiriwa kuwa asilimia 60 ya wakazi jumla ya wa Tanzania.
Bi. LULU amesema maeneo mengine yameshaanza kufaidika na Beki hiyo kwa vijana waliobahatika kukopeshwa pikipiki kwa masharti ya kuwasilisha shilingi laki tano na kupatiwa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.8, ambapo kijana atatakiwa kulipa kiasi kilichobaki kwa kadiri ya makubaliano.
Amefafanua kuwa kijana atawajibika kutoa fedha za fomu ambayo ni shilingi 20,000/=, a,bazo atalipa mara baada ya kuwepo na uhakika wa mzigo umeshawasili Bandarini ndipo wao uchukua hatua ya kumpigia simu yule kijana tayari ambaye amejaza fomu kumtaka aje na shilingi 20,000 za fomu na shilingi laki tano malipo ya utangulizi.
Mratibu huyo wa Benki ya vijana mjini Kibaha, BI. LULU MKOMAMBO ameongeza mbali ya kutoa mkopo wa pikipiki pia wamejipanga kutoa mikopo ya fedha ili kuwawezesha vijana wanaofanya shughuli tofauti kufaidika benki hiyo ambayo inamilikiwa na Jumuiya ya vijana ya Chama cha Mapinduzi.
END.
Comments
Post a Comment