X MAS
Ben Komba/Pwani-Tanzania/24-Dec-12/18:14:46
Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Pwani limesema kuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mkoa na halmashauri zake katika kipindi hiki cha Krismas ambapo leo kutakuwa na misa za mkesha tayari kwa sikukuu hiyo ya kuzaliwa mwokozi YESU KRISTO kama inavyoaminika na mabilioni ya wakristu ulimwenguni
Akiongea na mwandishi wa habari hizi msemaji wa Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani, INSPEKTA ATHUMAN MTASHA ambapo amesema siku kama hizi kunakuwepo na mikusanyiko ya watu wengi hasa maeneo ya makanisani na baa.
INSPEKTA MTASHA amewataka wazazi kutotoka wote majumbani kuepuka kutoa fursa kwa wahalifu kufanya madhara, na ameaasa kama watu watatoka itakuwa vyema anayebaki nyumbani kuwa na simu iwapo tatizo lolote litakalojitokeza atoe taarifa linapotokea tatizo.
Akizungumzia kuhusiana wenye magari amewataka madereva kupaki maeneo ambayo yapo salama na kuheshimu sheria za usalama barabarani katika kipindi hiki cha sikukuu kutokana na baadhi ya madereva ambao hutumia sikukuu kunywa kiasi kikubwa cha pombe na kusababisha ajali zisizo za lazima.
Msemaji huyo wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Pwani, INSPEKTA. ATHUMAN MTASHA akijibu swali kuhusioana na taarifa za vitisho za kutaka kulipua makanisa katika kipindi cha kismas kama ilivyonukuliwa katika vyanzo mbalimbali, amesema Jeshi la Polisi lipo imara na tayari kipindi chote na kutokana wao kujipanga vilivyo hakuna kitisho chochote ambacho kinaweza kuwashinda katika suala zima la kulinda usalama wa raia na mali zao.
END.
Comments
Post a Comment