ZING ZONG STORY
Ben Komba/Pwani-Tanzania/11-Dec-12/17:51:23
Mkazi wa Picha ya Ndege mjini Kibaha, BW. HEZRON MWANSASU amefikishwa mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mkoa wa Pwani akituhumiwa kwa kosa la kumuingilia kinyume cha maumbile mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 7 ambaye alikuwa anaishi naye.
Akisomewa shtaka mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mkoa, BW. ESTOMI KISANGA na Mwendesha mashtaka, BW. JONAS SIRA inadaiwa tarehe 24 Novemba mwaka huu majira ya saa tano usiku huko maeneo ya Picha ya Ndege mjini Kibaha mkoa wa Pwani mshtakiwa alimuingilia kinyume cha maumbile mtoto huyo mwenye umri wa miaka 7 ambaye jina lake limehifadhiwa na kumsababishia maumivu makali.
Hakimu mfawidhi wa Mkoa BW. ESTOMI KISANGA aliahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 21 Desemba mwaka huu na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.
END.
Comments
Post a Comment