CCM WAHIMIZA VIKAO VYA NDANI YA CHAMA.
Ben Komba/16 December 2012/23:32:44
Chama cha mapinduzi mjini Kibaha kimeonywa kuwa kisimtafute mchawi kitakapofanya vibaya katika uchaguzi mkuu ujao, kutokana na viongozi wa ngazi za matawi na Kata kutozingatia vikao vya kikatiba.
Mwenyekiti wa CCM, Kibaha mjini BW. MAULID BUNDALA amesema hayo akiwa katika ziara yake ya kukiimarisha chama katika kata ya Picha ya Ndege.
BW. BUNDALA amefafanua kutokana na mweleko anaona sasa kuna kila dalili ya viongozi na wanachama wa CCM wenyewe kuwa chachu ya kushindwa kwa chama hicho katika chaguzi zijazo.
Ameongeza toka mwanzo wa ziara yake amekatishwa tama na baadhi ya matawi kushindwa kuitisha vikao vya wanachama ili kuweza kutathimini utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama.
BW. BUNDALA ameyasifu matawi ya Picha ya Ndege B na Lulanzi kwa kuonyesha uhai wa chama katika maeneo hayo, na amewaonya viongozi ambao wamekuwa na tabia ya kutoroka vikao kwa visingizio mbalimbali.
END.
Comments
Post a Comment