MWENYEKIT UVCCM AKANUSHA UVUMI DHIDI YAKE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Friday, December 21, 2012/18:20:03 Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mjini Kibaha, BW.IDD KANYALU amekanusha uvumi wa kuwa yeye amekamatwa kwa jinai na kupelekwa Tanga kitu ambacho amethibitisha kuwa sio kweli. Akiongea na mwandishi wa habari hizi, BW. KANYALU amesema siasa ni mchezo mchafu na huwezi kumjua mbaya wako, na ameomba kama mtu yoyote ana madai kama hayo na athibitishe, kwani uchaguzi umemalizika hivi karibuni na makundi bado yapo. Bw.KANYALU amesema masuala hayo kweli yamezagaa katika lengo zima la kupakana matope kutokana na wanachama wa chama hicho kung'ang'ania makundi yaliyokuwapo wakati wa kampeni wa chaguzi za ndani za chama hicho, na kutokana na makundi kuna bomoa hali ya umoja na mshikamano iliyokuwepo hapo awali kabla ya mfumo wa vyama vingi kuingia nchini. Amewaasa wana CCM kuwa kitu kimoja na kuimarisha upendo na mshikamano ndani ya chama hicho, na si vyema kwa wanachama wa chama hicho kuchafuana kwa mambo ambayo hawana uhakika nayo, na linapotokea suala lolote ni vyema tukashikamana ili kuweza kukijenga chama bila kukaribisha majungu yasiyo na tija kwa chama. END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA