WATOA HUDUMA MAJUMBANI KIBAHA WALIA UJIRA KIDUCHU

watoa huduma kwa wagonjwa majumbani walia malipo hafifu kibaha Ben Komba/Pwani-Tanzania/15-Nov-12/05:30:05 PM Imebainishwa mijini Kibaha kuwa kubadilika kwa mashirika yanayoendesha mradi wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa majumbani mjini Kibaha, ndio chnazo cha kubadilika kwa taratibu mbalimbali za uendeshaji kutokana na kila shirika kuwa na sera yake. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kufuatia baadhi ya watoaji huduma kwa wagonjwa waliopo majumbani, kulalamikia ufinyu wa malipo ambayo wanapatiwa na shirika lisilo la kiserikali linalosimamia mradi huo kwa sasa mjini Kibaha la PATHFINDER kwa kushirikiana na RED CROSS na EGPF ambao wamerithi kutoka kwa shirika la KIFARU, Mratibu wa huduma za wagonjwa majumbani, DR. ALEX MLIGA amesema wadau hao wameanza kazi toka mwezi wa nne mwaka huu. Na kwa kuanzia waliendesha zoezi la utambuzi kubaini uwezo wa watoaji huduma majumbani waliopo, ili kubaini iwapo kama kuna wenye upungufu kutoendelea nao, na kigezo kikubwa kilichozingatiwa ni lazima mtoaji huduma ajue kusoma na kuandika, mtunza siri na awe mwanajamii wa eneo husika na mwajibikaji. DR. MLIGA amebainisha shirika kiongozi la sasa ambalo ni PATHFINDER mwongozo wake unaelekeza kuwa mtoa huduma majumbani anatakiwa awe amehizinishwa na kikao cha kitongoji au kijiji na ndipo apatiwe mafunzo na akiwa tayari kufanya kazi za kujitolea inapohitajika. Kuhusiana na ufinyu wa mallipo kwa wahudumu wa wagonjwa majumbani, DR. MLIGA amefafanua kuwa wahudumu walilipwa kufuatana na uwasilishaji wa ripoti zao kila mwezi na ndio sababu siku walipolipwa viwango vilitofautiana kutokana mhudumu mmoja kwenda kwa mwingine, kulinganisha na shirika la awali ambalo lilikuwa linasimamia mradi huo ambalo lilikuwa linalipa shilingi 30,000/= kwa mwezi na PATHFINDER wao wanawalipa shilingi 25,000/= kwa mwezi jambo ambalo linawanung'unisha watoaji huduma hao na hasa ikizingatiwa kupanda kwa hali ya maisha. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA