CCM INATISHA KIBAHA-KOKA

MBUNGE KIBAHA MJINI ASEMA CCM INATISHA-KOKA Ben Komba/Pwani -Tanzania/12/11/18/9:47:21 Mbunge wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SLYVESTER KOKA ametambia mafanikio ambayo Kibaha imeyapata katika kipindi cha miaka miwili akiwa kama mbunge wa Jimbo hilo. Akizungumza katika hafla ya kuwashukuru wananchi wa mtaa wa Kwa mfipa kwa kuichagua CCM karibuni katika nafasi zote za uongozi, BW. KOKA amesema katika kipindi cha miaka miwili cha ubunge wake amewezesha mji wa Kibaha kuwa na barabara ya lami kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa Kibaha kama makao makuu ya mkoa wa Pwani mwaka 1974. Mbunge huyo alipokuwa anawafumbua macho na masikio wananchi wa Kata ya Kwa mfipa kuhusiana na shughuli mbalimbali za maendeleo katika kipindi cha miaka miwili cha ubunge wake kwa kueleza nini kinaendelea, ikiwa pamoja na kuanzisha mfuko wa elimu wenye lengo la kuhakikisha vijana wanapata elimu ambayo itasaidia kuchochea maendeleo ya Jimbo lake. BW. KOKA amesema kuwa katika kuhakikisha mfuko huo unafanya kazi kama ilivyokusudiwa, amewaambia wananchi ni yeye ndiye atakayesimamia katika kuhakikisha wacahakachuaji hawapewi nafasi, aidha amebainisha mbinu ambazo atazitumia kupata fedha ni pamoja na kuhusisha wawekezaji lukuki wanaowekeza katika Jimbo hili. Hivyo mbunge huyo wa jimbo la uchaguzi Kibaha, BW. KOKA amewahakikishia wananchi wa wa Kibaha bila kujali chama gani kutembea kifua mbele kwani maendeleo yapo katika mwelekeo mwanana ambao utawezesha Mji wa Kibaha kuwa mji wa viwanda kutokana na kutengwa eneo maalum eneo la Zegereni ambalo zama hizo lilikuwa mashamba pori kuwa eneo la viwanda, lakini kwa sasa kumejaa wawekezaji kutoka nchini China. END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA