KAMPENI YA MAMA MISITU YAZINDULIWA PWANI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/11/11/12 Kampeni ya mama misitu imezinduliwa rasmi katika kijiji cha Kisanga tarafa ya Sungwi wilayani Kisarawe, ikiwa na lengo la kuahamasisha jamii kuwa na ufahamu kuhusiana na masuala ya utunzaji wa mazingira na umuhimu wake katika kupunguza hewa ukaa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo Mratibu wa BW. YAHYA MTONDA ambaye amesema lengo kuu la kampeni ya mama misitu, ni kupeleka suala la utawala bora katika suala la uhifadhi wa misitu kwa jamii ili kuweza kuwa shirikishi kwa jamii kushiriki moja kwa moja katika kuilinda na kuitunza misitu ya RUVU Kusini. BW. MTONDA ameongeza kuwa kwa kampeni hiyo ni kuleta mageuzi chanya katika suala uhifadhi wa misitu na kupunguza uvunaji haramu wa mazao ya misitu sawa na kuhakikisha wanajamii wanaoishi maeneo yaliyozunguka misitu wanafaidika kwayo. Amesema katika suala zima la kuwepo kwa utawala bora, halmashauri za wilaya na vyombo vinavyosimamia sheria kwa kuwapatia elimu kuhusiana na utawala bora katika suala zima la uhifadhi wa misitu. BW. MTONDA amebainisha kuwa kampeni hiyo inatekelezwa na washirika wenza 11, ambao wamegawanyika katika makundi mawili ya Taifa na wilaya katika ngazi ya taifa moja wapo ni MJUMITA, Trafiki maalum ambao wanakusanya taarifa mbalimbali kuhusiana na suala misitu, POLICY FORUM, LEAT, HEMINA na wengineo. Na katika ngazi ya wilaya utekelezaji unasimamiwa na shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania,katika wilaya za Rufiji na Kibaha kwenye msitu wa Ruvu kusini ambapo WSSP wanasimamia misitu ngazi ya wilaya ya Kisarawe, Mradi wa mama misitu unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 5. END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA