VUTA NIKUVUTE YA UDINI BADO YAENDELEA BAGAMOYO SEKONDARI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/03-Nov-12/17:25:09
Mgogoro wa kidini unaoendelea katika shule ya sekondari Bagamoyo na huku viongozi wa mkoa wa Pwani wakipiga chenga kuzungumzia suala hilo na kulishughulikia kutokana na wengi wao kuwa wenye madaraka makubwa mkoani hapa kuwa waumini wa dini ya Kiislam hali ambayo inaendelea kuzua maswali miongoni mwa wananchi hususan wakristo kuhusiana ni wapi tunakwenda.
Hayo yamezungumzwa na baadhi ya wazazi wa watoto wa kikristo wanaosoma kwa kuelezea kukatishwa tamaa na maneno ya Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani. SALEH MBAGA ambaye alikiri kwa kuwepo kwa tatizo hilo, na kuonysha kufurahishwa kwake na taarifa ya Mwalimu mkuu wa shule ya kuondoka na Familia yake kwa kusema wao ndio walivyotaka kwani wanafunzi wa kiislamu hawamtaki na ikizingatiwa kaimu kamanda naye ni muislam bila kuangalia wanafunzi wakristo wana hoja gani.
Mzazi huyo amesikitishwa na hatua ya serikali kujaribu kuvundika jambo hilo kwa kuficha taarifa kwa sababu ambazo hazipo bayana, na huku mgogoro huo ukichukua takriban miezi miwili, baada ya wanafunzi mamluki kupenyezwa shuleni hapo kupitia majina ya wanafunzi wakristo waliopasi na kuendelea na masomo kwenye shule bora zaidi.
Kutokana na Rais kuchagua viongozi wengi waislamu katika mkoa wa Pwani kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za nchi unaofanywa na waislamu bila kuchukuliwa hatua yoyote ikiwa pamoja na uporaji wa kiwanja namba 64 katika kitalu B Kilichopo mjini Kibaha cha Mjane wa Kikristo wakisaidiwa na viongozi wa juu wa mkoa na serikali kuu kama wanavyojitapa kwamba wao ndio wao na hakuna wa kufanya lolote.
Kana kwamba haitoshi Waislamu wamekuwa wakituma vijana wao katika mazishi ya Kikristo kwenda kufanya fujo jambo ambalo hapo nyuma halijawahi kushuhudiwa na hali hii ikiashiria kufikia kilele cha amani yetu kutokana tu na baadhi ya watu ambao kwa njia moja ua nyingine wanaonekana kuchekewa wakiwa wanahatarisha amani ya nchi kama ilivyoshudiwa katika misa ya mazishi ya Bint ROSEMARY KAJUWALA ambayo iliongozwa Padri. ROMWARD MKANDARA wa Parokia ya Tumbi mjini Kibaha.
Akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na mgogoro huo mara baada ya mkutano nao, Mkuu wa mkoa wa Pwani BI. MWANTUMU MAHIZA amedai mgogoro huo eti ni wa enzi na enzi toka yeye akiwa waziri wa elimu, ingawa kuna baadhi ya wanafunzi wanaosoma hapo wamesema mgogoro umezuka kufuatia wanafunzi kutoka NDANDA Sekondari ambao wakorofi walipohamishiwa shuleni hapo.
END.
Comments
Post a Comment