ONLINE BENEFITS
Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/11/23/8:53:32 AM
Mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI. MWANTUMU MAHIZA ameelezea matarajio makubwa ya mafanikio katika suala zima la maendeleo kutokana na kujengwa mkonga wa mawasiliano wa Taifa na hivyo kurahisisha utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari ambao walikuwa wameambatana na na mtaalamu wa masuala ya Mtandao, BW. LUKELA MKAMI ambae alikuwepo hapa kwa ajili ya kuwanoa waandishi wa habari wa mkoa Pwani juu ya matumizi ya mtandao wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Ambapo Mkuu wa mkoa MAHIZA amesema yeye binafsi amefurahishwa na hatua ya serikali kujenga mkonga wa mawasiliano ambao unanuwiwa kupunguza gharama za matumizi ya mtandao na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya serikali.
Amebainisha mpaka sasa serikali imeshaanza kutekeleza majukumu yake mbalimbali kwa kutumia mtandao ikiwa pamoja na kuanzisha ulipaji wa fedha kwa kutumia mfumo wa kielektroniki unaojulikana kama EPICOR, ambapo badala ya mhasibu kubebelea fedha mkononi basi fedha zitamfikia alipo kwa njia ya mtandao.
BIBI. MAHIZA amelezea hatua ambayo mpaka sasa ofisi yake imeshachukua katika kuhakikisha wanafaidika na huduma ambayo itatolewa kutokana na kukamilika kwa mkonga wa Taifa wa mawasiliano, kwani hapo baadaye atakapotaka kutoa taarifa mbalimbali atakachofanya ni kwenda kwenye chumba kitakachokuwa na vifaa maalum na kutoa taarifa yake ambayo itasambaa kwa haraka.
BW. LUKELO MKAMI ambaye ni mtaalamu wa mtandao amesifu hatua zilizochukuliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani, ya kuona umuhimu wa matumizi ya mtandao katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya serikali, na ameitaka serikali kuhakikisha wanasaidia kuifikisha huduma hiyo maeneo ya pembezoni ili kuhakikisha malengo yanafikiwa kabla ya mwaka 2025.
Mafunzo hayo ambayo yametolewa kwa waandishi wa habari 18 wanaokaa na kufanya kazi zao, katika mkoa wa Pwani, ambayo yametolewa na muungano wa klabu ya waandishi wa habari Tanzania UTPC na kufadhiliwa na shirika la misaada ya kimaendeleo la SWEDEN, SIDA.
END.
Comments
Post a Comment