CHANJO MPYA YA NIMONIA NA ROTAVIRUS WANACHI WAHAMASISHWA.




Ben Komba/Pwani-Tanzania/30-Nov-12/06:27:06


Wananchi wilayani Kibaha wametakiwa kuto ushirikiano wa kutosha kwa watoa huduma ya chanjo ROTAVIRUS na NIMONIA katika suala zima la uimarishaji wa afya, na katika muda wote wa utekelezaji wa zoezi hilo ambalo likifanikiwa litawezesha kufanya magonjwa ya uti wa mgongo na kuharisha kwa watoto wadogo kuwa historia hapo baadaye.


Akizungumza katika kikao cha uhamasishaji na kamati ya afya ya msingi ya wilaya, Mwakilishi wa mkuu wa wilaya Bw. ANATOLY MHANGO amekemea tabia ya baadhi ya watu kupotosha malengo ya chanjo mbalimbali zinazotolewa kwa jamii katika kuiepusha na magonjwa ambayo yanaweza kukingika.


BW. MHANGO amewaasa wananchi kutoa ushirikiano ili kuweza kiampeni hiyo ya chanjo ya RITOVIRUS na NIMONIA ifanikiwe, katika kuhakikisha suala zima la kuboresha huduma ya afya ya jamii.


Naye Mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BIBI. REHEMA PILIMO amesema kuwa ROTAVIRUS ni vimelea vinavyosababisha kuharisha kwa watoto chini ya miaka 5, kiasi cha asilimia 40 ya watoto walio chini ya mwaka mmoja hasa kati ya miezi 6 na 11 huambukizwa ugonjwa wa kuharisha husababisha upungufu mkubwa wa maji mwilini.


BIBI, PILIMO ameongeza kuwa  Virusi vya ROTA huenezwa kwa njia ya kula au kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye virusi hivyo, na dalili kubwa za ugonjwa huo ni kutapika, kuharisha kunakoweza kuchukua siku 4-7, kupungukiwa majimwilini, homaa, utapiamlo na kudumaa sawa na mtindio wa ubongo.


Naye Mratibu wa afya ya uzazi ya mama na mtoto halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BI. MARIA KAHEMA akizungumzia kuhusu chanjo ya NIMONIA, Amesema  ugonjwa huo husababishwa na vimelea aina ya STREPTOCOCCUS PNEUMONIAE ambavyo husababisha magonjwa mengi yanayoweza kuua kwa haraka kamaUti wa mgongo, uambukizo wa bakteria kwenye damu, sawa magonjwa ya masikio, pua na mapafu.


BI. KAHEMA ameeleza jinsi ugonjwa huo ambao unasambazwa kwa njia ya hewa mtu mwenye ugonjwa anapopiga chafya au anapokohoa na kwa kugusa leso ambayo imetumiwa na mgonjwa mwenye matatizo hayo, Kampeni ya uzinduzi wa chanjo hiyo kitaifa unatarajiwa kufanyika DESEMBA 03 Mwaka huu.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA

WANANCHI KIDIMU WAPINGA HATUA YA MKURUGENZI WA MJI KIBAHA.