UPATIKANAJI WA MAJI KUBORESHWA-KIBAHA.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/18:38/27-11-2012.


Chanzo cha maji chenye uwezo wa kuzalisha mpaka zaidi ya mita za ujazo 36,ambazo ni sawa lita 36,000 za maji zinazalishwa na chanzo cha kisima kilichochimbwa maeneo ya Ngeta katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha, na kuvifaidisha vitongoji 6 vya halmashauri vya halmashauri hiyo.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mhandisi wa maji katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW. CHRISTOPHER MDUMA amesema hatua hiyo ni katika kuhakikisha halmashauri ya wilya ya Kibaha inakuwa na maji ya uhakika katika kipindi chote cha mwaka.


BW. MDUMA ameongeza chanzo cha maji cha Ngeta kitawezesha kupunguza makali ya upatikanaji wa maji kwa baadhi ya vitongoji ambavyo awali iliwalazimu wakazi wake kutembea umbali mrefu kutafuta maji hasa nyakati za kiangazi, kutokana na visima vingi kukauka katika kipindi hicho.


Amefafanua kuwa kabla ya kutekelezwa kwa mradi huo, wananchi walikuwa wakitegemea visima vya asili, kutokana na chanzo cha Ngeta kitafaidisha vitongoji vya, Ngeta, Msongola, Mwanabwito, Disunyara, Lupunga na Kikongo.


Mbali na chanzo hicho, Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW. MDUMA ameleeza kuwa baadhi ya  vitongoji vya Soga na Vikuge hivyo vinafaidika moja kwa moja na maji ya DAWASCO, na huku vitongoji vya Vikuruti, Dossa Aziz na Mihande nao wafaidika na maji kutoka bomba la DAWASCO.


Katika kutekeleza hilo, BW.MDUMA amebainisha juhudi mbalimbali zinafanyika katika kuboresha upatikanaji wa maji ya uhakika, kwa kujenga bwawa katika eneo la Kidunda, Morogoro vijijini ambalo litaboresha upatikanaji wa maji katika wilaya mbili za mkoa wa Pwani za Bagamoyo na Kibaha.


Kwa kutumia Bwawa la Kidunda, maji ya mvua yatakusanywa na kuzuia kwa kuwekwa matuta maalum yatakayozuia maji kusambaa hovyo nyakati za mvua, ili kuweza kutumika kipindi cha kiangazi.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA

WANANCHI KIDIMU WAPINGA HATUA YA MKURUGENZI WA MJI KIBAHA.