KIBAHA INDEPENDENT SCHOOL.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/10/07/12:04:46 PM Shule ya msingi ya Kibaha independent iliyopo mjini Kibaha imeazimia kuwaandaa wanafunzi kuishi kulingana na maendeleo na mabadiliko ya sayansi ya teknolojia ya utandawazi ili kuweza kukua kitaaluma, kiakili, kijinsia na kimaono. Ameyazungumza hayo Mkuu wa shule ya Kibaha Independent, BW. HEZRON MUSALALE wakati akimkaribisha mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la saba, Lengo kuu la shule yao ni kuhakikisha vijana wanaopita hapo wanakuwa matunda ambayo yatachangia kwa njia moja au nyingine maendeleo ya Taifa. BW. MUSALALE amebainisha makakati wa shule kuvipa nuru ya kielimu vizazi vingi kwa kuvipatia elimu ya hali ya juu, na hasa shule ikiwa ina malengo mahsusi ya kuhakikisha wanafunzi wanaweza kusoma na kuandika kwa kutumia lugha mbalimbali hususan Kiswahili na Kiingereza, kuhakikisha wanafunzi wanajenga uwezo wa hali ya juu ya mahesabu na pamoja na kuwajenga wanafunzi katika kujiamini na kuwa na mawazo yakinifu. Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa chuo cha wananchi Kibaha, BW. CHARLES MLATA amesema juhudi ambayo wameifanya katika kulea watoto kimaadili na kitaaluma kama walimu waliyotuambia inajidhirisha wazi na matokeo ya mitihani yanayopatikana hapo ambapo kwa vipindi viwili vilivyopita imeonekana kuimarika. BW. MLATA amemsihi mmiliki wa shule hiyo ALHAJI YUSUPH MFINANGA kuifanyia kazi risala ya wanafunzi wanaomaliza ambao wameomba kuongezwa kwa vitabu katika maktaba ya shule, kuhakikisha kunakuwepo na programu za kutosha za kompyuta ili wanafunzi waweze kujifunza vizuri, na kununuliwe basi kwa ajili kubeba wanafunzi kutokana na yaliyopo kutotosheleza na aidha wameiomba menejimenti ya KIBAHA ENGLISH MEDIUM INDEPENDENT SCHOOL kujenga shule ya Sekondari ili wazilazimike kuacha mazingira hayo pindi wamalizapo elimu ya msingi. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA