KINAMAMA WAWEZESHWA NA INUKA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-Oct-12/4:56:04 PM Wafanyakazi ambao wameajiriwa katika sekta mbalimbali za utumishi wa umma wametakiwa kujishughulisha na masuala ya ujasiria mali wanapotoka kuwajibika katika kazi zao walizoajiriwa nazo ili kuweza kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambazo wanakumbana nazo kwa sasa na mara baada ya kustaafu. Mkurugenzi mtendaji wa kanda ya kaskazini, BW. DAVID MSUYA wa shirika hilo linaloitwa INUKA, linalowawezesha kina mama wajasiriamali bila kulazimika kuwa na amana kama ilivyo kwa taasisi nyingine za fedha, amesema katika kanda yake kuna vikundi takriban 24 na lengo kuu ni kuwajengea uwezo akinamama kuweza kutambua haki zao za msingi na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali ili kumfanya Mama nae awe chanzo cha mapato. BW. MSUYA amesema katika Mkoa wa Pwani wameanza kwa ktengeneza vikundi viwili ambavyo kimoja kipo katika Kata nya Magomeni mjini Bagamoyo na kingine kikiwa Ruvu darajani, amebainisha vikwazo kadhaa kujitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo, hasa katika kata ya Magomeni kwa baadhi ya watu kugoma kurejesha mikopo hiyo wakidai ni zawadi kutoka kwa Rais ambaye ni mwenyeji wa Bagamoyo. Ameongeza kuwa katika Kata hiyo ya Magomeni watu 267 walifaidika na mikopo hiyo na kati ya hao watu 30 walitoroka wakiwa wanadaiwa na kuhamia katika maeneo mengine hali ambayo inawakatisha tamaa, na kutokana na hali hatua kadhaa wamazimia kuzichukua ikiwa pamoja kuwafikisha mahakamani wadaiwa sugu ili waweze kurejesha fedha walizopeshwa na kutoa fursa kwa wengine kukopeshwa. BW. MSUYA amezungumzia kuwepo kwa mafanikio katika baadhi ya maeneo kama Kata ya Mbuyuni iliyopo Morogoro eneo ambalo walifanya vizuri tofauti na ilivyokuwa wilaya ya Mvomero ambako wamepata hasara ya takriban shilingi milioni 19 kutokana na wakopeshwaji kushindwa kurudisha mkopo huo na hivyo kuathiri wajasiamali wengine ambao walikuwa wanahitaji huduma hiyo. Mkurugenzi huyo Kanda ya kaskazini wa INUKA, BW. DAVID MSUYA amewashukuru wafadhili wao GLOBAL HEAT wa DENMARK kwa kuwawezesha kuendesha zoezi hilo la kuwajengea uwezo wa kifedha wakinamama wajasiriamali ili waweze kujikwamua kutoka katika dimbwi la umaskini. END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA