MJI WA KIBAHA WAPANGA MIKAKATI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/28-Oct-12/10:56:35 Halmashauri ya mji wa Kibaha katika robo ya kwanza ya Julai-Septemba inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 4 milioni 230 laki mbili elfu 15 na 94, ikiwa ni makusanyo kutoka vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ambayo ni asilimia 36 ya makisio ya mwaka 2012 mpaka 2013. Akisoma taarifa hiyo Makamumwenyekiti wa halmashauri hiyo BW. NANGULUKUTA SAID AHMAD amebainisha halmashauri katika robo ya kwanza ya Julai mpaka Septemba 2012 inatarajia kutumia shilingi milioni 323,967,413/= ambayo ni sawa na asilimia 16 ambayo ndiyo ya makisio ya mwaka wa fedha 2012/2013 ikiwa pamoja na salio anzia la Julai 01 2012. Na kati ya mambo ambayo yanatarajiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na suala zima la utunzaji na usafi wa mazingira ya mji wa Kibaha kwa kuzindua gari la taka kwa ajili ya kukusanya taka kutoka maeneo mbali, kipaumbele kingine kitakuwa ni ununuzi wa gari la idara ya ardhi kupitia mapato ya ndani. Akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibaha,, BW. MAULID BUNDALA amewaambia watendaji na madiwani kufanya shughuli zao kwa umakini ili kuepusha na kutangaza shughuli ambazo zimetekelezwa na halmashauri ili kuwapa wananchi fursa ya kujua juu ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo. Amesema halmashauri imekuwa ikifanya miradi mbalimbali lakini kutokana na halmashauri kutotoa taarifa juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo inayotekeleza ili kupunguza manun'guniko kutoka kwa wananchi ambao wanahitaji taarifa kutoka kwa watendaji na madiwani wa halmashauri ya Mji wa Kibaha. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA