UDINI WAFUKUTA BAGAMOYO SEKONDARI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-Oct-12/16:14:56 Hali ya sintofahamu imeyakumba mazingira ya Shule ya sekondari Bagamoyo kufuatia wanafunzi wa Kiislamu kutaka shule hiyo iendeshwe kwa misingi ya Kiislamu, na wakisusia taratibu za kawaida za shule kwa kisingizio cha kutekeleza nguzo za Kiislamu ya Uislam wao kwa kuamua kumlazimisha Mwalimu Mkuu aachie nafasi hiyo eti kuwa amekuwa akiwanyanyasa sana wao. Kutokana na hali hiyo wanafunzi wa Kikristo nao wakaamua kuvunja ukimya kwa kuamua kukabiliana na wanafunzi wenzao wa Kiislam ambao walikuwa wanataka kumshambulia Mwalimu Mkuu kwa kumsogelea na kumweka kati, na kuona hivyo wanafunzi wakristo nao wakasogelea eneo hilo wakiwa wamewazunguka Wanafunzi hao Waislamu wakiawaangalia kujua watamfanya nini Mwalimu Mkuum ili kujibu mapigo dhidi ya wenzao wa Kiislamu. Taarifa ya chanzo chetu ndani ya eneo la tukio kinasema hali hiyo imefuatiwa kwa kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi kama ilivyo ada, na ndipo ilipobainika kuwa wenzao Wanafunzi wa Kiislamu walikuwa wameaanda mikakati yenye harufu ya udini kama ilivyo katika chaguzi nyingi zinazoendelea hivi sasa nchini, kuona mbinu zao zimegundulikja wanafunzi hao wa Kiislamu wakaamua kususia uchaguzi. Kutokana na uongozi kubaini hilo haukungojea mpaka wanafunzi hao wacheke ndipo taratibu za kimsingi za kupata viongozi wa wanafunzi ziendelee uchaguzi ulifanyika washiriki wakiwa wakristu pekee yao na kunyakua nafasi mbalimbali, Lakini kama Waswahili walivyobaini kuwa wanafunzi hao wa Kiislamu walikuwa na kisebusebu na kiroho papo kutokana na wao kuazimia kufanya fujo kwa lengo la kuzuia kuapishwa kwa viongozi hao. Kutokana na hali kuwa tete huku wanafunzi wakristo wakieleza bayana kuchoshwa na vitimbi vya wenzao ambao kila kukicha wamekuwa wakizua chokochoko badala ya kuzama katika masomo, kwani wamefikia hatua ya wanafunzi wa Kiislamu kutaka kulala mabweni ya pekee yao, mambo hayo yameshika kasi sana mjini Bagamoyo toka Rais JAKAYA KIKWETE ashike madaraka ya kuongoza nchii hii na kuacha maswali mengi miongoni mwa watanzania. Taarifa za uhakika zinabainisha kuwepo kwa mapandikizi ya wanafunzi ambao wamebeba agenda ya maangamizi moyoni mwao kama ambavyo wamesikika wakati wa sakata hilo kwamba lazima waue mtu, na kufikia hatua ya kumnyang'anya Mkuu wa shule Karatasi aliyoshika mkononi na kuichana, Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya tayari imefika shuleni hapo kujaribu kurekebisha hali ya mambo, Ingawa kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa kikristo juu ya tabia ya Afisa elimu Sekondari kufika shuleni na kuongea na Waislamu pekee yao na hatua ya yeye kuruhusu msikiti shuleni hali inayowasababishia makelele wanapotaka kujisomea. Nilifanikiwa kumpata msemaji wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani INSPEKTA. ATHUMAN MTASHA ambaye amekiri kuwepo kwa tukio hilo, lakini kwa kipindi hicho hakuwa eneo la tukio hivyo hakuwa na taarifa ya kutoa mpaka hapo baadaye. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA