VITA VYA KIDINI VYAPEWA NAFASI BAGAMOYO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/28-Oct-12/09:35:52 Wanafunzi wakristo wa shule ya Sekondari Bagamoyo zamani maarufu kama MAGAMBANI wamefunga virago vyao na kuamua kurudi makwao kufuatia serikali kushindwa kusimamisha uasi unaofanywa na wanafunzi wa Kiislam wanaosoma katika shule hiyo ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwakashifu wenzao wakristo na kuwatishia kuwauwa huku wakiangaliwa tu. Mmoja wa wanafunzi ambaye amerejea jana kutoka shule hiyo kutokana na hali kuzidi kuwa tete kutokana na kutochukuliwa hatua madhubuti ya kutatua mgogoro huo na serikali ya wilaya ya Bagamoyo inayoongozwa na BW. AHMED KIPOZI ambaye amewahi kuwa mwandishi wa habari na Mhadhiri katika Chuo cha Kiislam Morogoro kushindwa kutatua mgogoro huo ambao umeota mizizi wilayani hapo. Wanafunzi hao waliamua kuondoka kufuatia baadhi Waislamu wa nje kushupalia mgogoro huo na kuwatisha wanafunzi wakristo hao ambao wengi wao wakiwa ni wenye umri wa miaka 18 mpaka 25, ambapo nao wameazimia iwapo serikali itakubali ulalamishi huo wa wanafunzi wa kiislam wa kutaka Mwalimu mkuu huyo aondolewe kwa kuwa ni mkristo na aletwe musilamu mwenzao basi wao wapo tayari kuhama shule kwani haiwezekani mtu akataka Mwalimu wa dini yake kuna agenda gani ya siri. Juhudi ya Mwalimu mkuu wa shule hiyo BW. BONUS NDIMBO kuwasihi wanafunzi hao wa kikristo wasiondoke ziligonga mwamba na kumueleza kuwa wao hawana imani na serikali ya wilaya ya Bagamoyo na serikali kuu ambayo kwa takriban wiki mbili wanafunzi hao wamekuwa wakifanya vurugu na kutishia maisha ya wenzao ikiwa pamoja na kuzuia walimu kuingia madarasani, hivyo wao kuona hakuna sababu kukaa sehemu kama hiyo ambayo wahuni wameshika hatamu. Shule ya sekondari Bagamoyo ipo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ambayo zamani ilikuwa inajulikana kwa jina la MAGAMBANI Sekondari, inakadiriwa kuwa na wanafunzi zaidi ya 700 kati ya hao wanafunzi waislamu ni 200 tu na ndio wao wamekuwa chanzo cha vurugu shuleni hapo wakishirikioana na raia wa nje ambao wamekuwa wakifika shuleni hapo nyakati a usiku kuanga mipango ya mkuendeleza uasi wao. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA