WAJASIRIAMALI VIJANA WAONYESHA BIDHAA KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/10/07/11:05:32 Waziri wa utamaduni, habari, vijana na michezo BIBI. FENELA MKANGARA amewahimiza vijana kujikusanya katika vikundi kwa lengo la kujiendeleza katika kazi za kijasiriamali kwa kuwawezesha kuaminika katika umoja wao na kuweza kukopesheka kwa kudhaminiana wenyewe kwa wenyewe. BIBI. MKANGARA amesema vijana kwa kujikusanya katika vikundi na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali kutasaidia kwa kiasi kikubwa vijana wanaoamka na kukaa vijiweni bila kujishughulisha na kazi yoyote ya uzalishaji mali, na kuwataka vijana kutumia kilimo kwanza kujiajiri binafsi na hasa kutokana na maisha ya sasa kuhitaji vijana kuwa wabunifu ili waweze kujiepusha na umaskini. BIBI. MKANGARA amewahimiza kila kijana wa Kitanzania kuanzia miaka 18 aweze kuchangia chakula mezani kwao kwa kuwajibika kikamilifu katika shughuli za kijasiriamali ambazo zitawaingizia tija, na Wizara ya utamaduni, habari, vijana na michezo itajitahidi kwa hali na mali kutafuita masoko kwa ajili ya bidhaa ambazo zitazalishwa na wajasiriamali. Amefafanua kuwa mtazamo wa serikali mbalimbali duniani unalenga katika uimarishaji wa sekta binafsi ili kutoa fursa kwa sekta hiyo kuchangia kipato cha serikali na kupunguza pengo la ajira lililopo kwa sasa kwa vijana. Mratibu wa maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na mtandao wa vijana wajasiriamli mkoa wa Pwani wa RIGHT TIME wenye maskani yake katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi, BI. TUNSIIME KYANDO amesema mtandao huo mpaka sasa umeshatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana takribani 350. BI. KYANDO ameweka wazi kuwa vijana wenye umri kati ya mikaka 15-35 waliopo katika mkoa wa Pwani ni asilimia 13 ambao wanajishughulisha na kilimo, na kundi hilo ndio wanaotarajiwa kuwa wazalishaji waku wanaendelea kuwa tegemezi ili hali kuna maeneo makubwa yaliyo wazi kwa ajili ya kilimo, hivyo klupitia mpango wa KAZI NJE NJE wamewawezesha vijana kujitambua na kuwapatia mbinu ya kutumia fursa zinazowazunguka badala ya kujikalia bila shughuli ya uzalishaji mali. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA