TTCL PWANI YAIBIWA NYAYA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/19/12/18:56:24
Shirika la simu katika Mkoa wa Pwani -- TTCL-- limekumbwa na wimbi la kuibiwa nyaya za kusambazia miundombinu ya simu katika Maeneo ya mamlaka ya mji wa Kibaha na wilayani Kisarawe na hivyo kuathiri utoaji wa huduma hiyo ya mawasiliano kwa simu za waya.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini Kibaha, Meneja wa TTCL mkoa wa Pwani, BW. FRANCIS MWENDA amesema kuwa wizi huo uetokea maeneo ya TAMCO kati ya Agosti 11 mwaka huu majira ya saa 1.30 na saa 2.00 na kuathiri wateja takriban 30.
BW. MWENDA ameongeza waya ulioibiwa ulikuwa na urefu wa mita 180, ambapo mtuhumiwa amekamatwa japo anajifanya hamnazo anapotakiwa kujitambulisha kwa kutaja majina tofauti kila wakati, na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
Aidha BW. MWENDA amefafanua kwamba matukio hayo ya wizi yamekuwa yanashika kasi kiasi cha kusababisha wilaya ya Kisarawe kukosa mawasiliano kw karibu wiki mbili sasa kutokana na hujuma ambayo imefanywa na watu wasiojulikana ambao wameiba kipande kikubwa cha nyaya zinazotumika kusambaza mawasiliano.
Meneja huyo wa TTCL Mkoa wa Pwani, BW. PETER MWENDA amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wanapomuona mtu akiharibu kwa nmakusudi miundombinu ya simu, kutokana na vitendo hivyo kuiletea kampuni hasara kwa kulazimika kununua nyaya hizo mara yanapotoikea matukiuo ya wizi ili kuwawezesha wateja kupata huduma endelevu.
Inasemekana kuwa wizi wa waya hizo za simu kunaendeshwa na wafanyabiashara wakubwa ambao kwa kuwatumia cvijana ambao wana maisha magumu wamefanikiwa kuwashawishi na kuwaingiza katika klujishughulisha na wizi wa waya za simu kwa lengo la kupata waya za madini ya shaba ambazo wanaziyeyusha na kuziuza kwa kilo moja kwa wastani wa shilingi za kitanzania kati ya 7000/= na 10,000/=.
END.
Comments
Post a Comment