MAMA WA KAMBO ATESA MWANA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/2012-09-30/09:21:22
Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Mlandizi, BI. MIRIAM MBWANA amemuhukumu muuguzi BI. JOSEPHINE CHARLES wa kituo cha afya Mlandizi kilichopo katika wilaya ya Kibaha, kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki mbili na fidia ya shilingi 150,000/= kwa ajili ya kumtesa mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 6.
Akitoa hukumu hiyo HAKIMU MBWANA amesema kufuatia uwepo sheria ya haki ya mtoto ambayo inasisitiza katika kumlinda na kumpatia haki stahili mtoto na si vinginevyo, kutokana na hilo hakimu huyo ameamuru mtoto huyo ambaye jina limehifadhiwa akabidhiwe kwa Afisa ustawi wa jamii BW. SAID MBEGU mpaka hapo mama yake mzazi atakapopatikana.
Hali hiyo inafuatia wakazi wa mtaa wa Kaloleni uliopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi kuungana kunusuru maisha ya mtoto wa kambo, Ambaye mumewe BW. CHARLES JULIUS DINDA amezaa na mama mwingine, na yeye kumpata BI. JOSEPHINE CHARLES ambaye amezaa naye mtoto mmoja ambaye ana miezi 6.
Mume huyo wa BI. JOSEPHINE ambaye inasemekana anafanyakazi mjini DAR-ES-SAALAM na kumuacha mtoto wake na Mama yake wa kambo, kwa mujibu wa majirani amekuwa akimtendea visivyo mtoto huyo kwa kumuadhibu kiasi cha kumtoa makovu maeneo mbalimbali mwilini.
Mmoja wa mashuhuda wa mateso ambayo alikuwa akiyapata mtoto huyo kabla ya uongozi wa mtaa wa Kaloleni kuingilia kati kumwokoa, ameshangazwa na tabia ambayo imeonyeshwa na muuguzi huyo ambaye anatakiwa kuwa mwenye huruma na upendo ili kutimiza wajibu wake badala ya kuwa katili wa mfano.
END.
Comments
Post a Comment