MJI WA KIBAHA KUFAIDIKA NA USHIRIKIANO

Ben Komba/Pwani- Tanzania/9/17/12/19:00:02 Ushirikiano uliopo kati ya halmashauri ya mji wa Kibaha na manispaa ya manispaa ya mkoa wa kisiwa cha GOTLAND, utainufaisha kwa kiasi kkubwa katika suala la demokrasia na, usambazaji wa maji safi na salama, utunzaji wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisisni kwake mjini Kibaha, Mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. ABUDADI MKOMAMBO amesema uhusiano huo kati ya miji hii miwili una takribani miaka 12 sasa. Ambapo BW. MKOBAMBO amebainisha katika kipindi cha miaka miwili ijayo yaani m,waka 2012 mpaka 2014, uhusiano wao umetoa kipaumbele kwa miradi kadhaa ambayo itafadhiliwa na ICLD (international center for loca demokrasi) ambayo ina lengo la kuimarisha demokrasia kwa watu wa kada ya kawaida, ikiwa pia ndio kipaumbele cha shirika la kimataifa la maendeleo la SWEDEN-SIDA- Akizungumzia suala la kuimarisha mfumo wa maji halmashauri ya mji wa Kibaha itaanzisha miradi mipya ya usambazaji wa maji na kuitekeleza kutokana na usaidizi wa manispaa ya GOTLAND, ikiwa pamoja na uimarishaji wa mfumo wa awali wa mtandao wa mabomba ya maji na matengenezo sawa kujengwa kwa viosk vya maji safi. Mbali ya utekelezaji wa mambo hayo, Halmashauri ya mji wa Kibaha itafaidika na uanzishwaji wa mpango maalum ya kuimarisha mazingira ya kazi za ukusanyaji, urudufishaji taka (recycling) na hatimaye kuharibu uchafu husika, kwa kuziweka katika makundi maalum. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA