SENSA YAANZA PWANI NA ONYO KWA WAKOROFI.
BenKomba/Pwani-Tanzania/Sunday, August 26, 2012/19:38:46
Zoezi la sensa ya watu na makazi limeanza rasmi Katika mkoa wa Pwani na kuwepo na vipingamizi vidogo vidogo vilivyojitokeza na na kushughulikiwa na viongozi katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa manufaa ya Taifa.
Leo ii mwandishi wa habari hizi ameshuhudia Mkuu wa mkoa wa Pwani BIBI. MWANTUMU MAHIZA akihesabiwa kama ilivyo ada inapofikia siku hii muhimu kitaifa, Ambapo baada ya kuhesabiwa amesema kuwa anajisikia fahari kuhesabiwa kwani anatambua kwamba yeye kuwa ni mtanzania halisi na wala sio suala la kuchosha na haijateteresha imani yake ya dini.
Na amewataka wananchi kujitokeza kuhesabiwa bila kujali kampeni zinazoendeshwa na watu wasio itakia mema Tanzania kwa kivuli cha udini, Ingawa mpaka sasa hakuna vikwazo vyovyote ambavyo vimejitokeza, toka ulinzi wa kutosha uliwekwa katika maeneo yote ambayo yalikuwa na utata.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Pwani BIBI. MAHIZA amewataka makarani wa sensa kuwa makini wakati wa utekelezaji wa majukumu yao na kuepukana na vitendo vya ulevi ambavyo vinaweza kuathiri zoezi hilo kama ilivyotokea mkoani Ruvuma ambapo karani mmoja alikwenda kugida ugimbi na madododso marefu na mafupi na hatimaye kuambulia kuyapoteza madodoso hayo.
BI.MAHIZA amesisisitiza kuwa sheria inafuata mkondo kwa yeyote ambaye atajaribu kuhujumu zoezi hilo adimu ambalo linakusudia kupata takwimu halisi ya Watanzania kila baada ya miaka kumi.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani amelazimika kusafiri kwenda wilayani Rufiji kutokana na kujitokeza uzembe katika utekelezaji wa zoezi hilo na kusababisha kutolipwa kwa makarani wa sensa ya watu na makazi mpaka leo hii.
END.
Comments
Post a Comment