KIBAFA KUJADILI UCHAGUZI JUMAPILI
KAMATI YA UTENDAJI KIBAFA KUKETI
Na Omary Mngindo, Kibaha
Agosti 10
KAMATI ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani inataraji kuketi Jumapili wiki hii kujadili mambo mbalimbali ya chama hicho.
Hayo yameelezwa na Katibu wa chama hicho Kidodo Seif wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa ambapo amesema kikao hicho pia kitazungumzia masuala ya uchaguzi unaotaraji kufanyika hivi karibuni.
Alisema kwamba tayari uongozi unaomaliza muda wake umeshafanya maandalizi yote ya uchaguzi na hivi sasa wanasubiri tarehe itapokuwa imefika ili zoezi hilo lfanyike na hatimaye viongozi wapya waweze kupatikana.
“Chini ya Mwenyekiti wetu wa Kamati ya uchaguzi David Silaha tayari mchakato mzima wa zoezi hilo umekamilika ambapo wanamichezo zaidi ya 25 wamneshachukua fomu na kurejesha,” alisema Kidodo.
Katibu huyo amewaomba viongozi wa KIBAFA kufika kwenye kikao hicho ili kupanga mikakati ya uchaguzi huo ambao unataraji kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu Kibaha (UMOVIKI) Mrisho Khalfan amesema kuwa vilabu vimeshajipanga kuhakikisha wanafanya uchaguzi huo kitaalamu zaidi na kupata viongozi wataoliendeleza soka la Kibaha.
“Viongozi wapo tayari katika mchakato wa kupatkana kwa viongozi wa KIBAFA kwa lengo la kuendelezwa kwa soka la Kibaha na Mkoa kwa jumla,” alimalizia Mwenyekiti huyo.
MWISHO.
Comments
Post a Comment