BODABODA PWANI WATAKIWA KUJIPANGA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/09/08/2012 12:20:06
Wanajeshi na Polisi wanaomiliki pikipiki zinazofanya shughuli za
uchukuzi wa abiria katika maeneo mbalimbali ya halmashauri ya mji na
wilaya ya Kibaha wametakiwa kuheshimu taratibu ambazo zimewekwa na chama cha
waendesha bodaboda mjini hapa.
Akizungumza na waendesha pikipiki wa mjini Kibaha afisa tawala wa mkoa
wa Pwani, BI. BEATHA SWAI katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani,
amesema wao wanajeshi na Polisi wanatakiwa kuwa mfano bora katika
kuheshimu taratibu zilizopo badala ya kutumia nafasi zao katika jamii
kufanya mambo kinyume.
Hivyo amewataka wamiliki hao kuwaongoza madereva wao katika
kuwasisitizia kuheshimu taratibu za chama cha waendesha bodaboda na
uongozi uliopo ili kuwezesha kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kwa
kuzingatia taratibu zilizopo.
BI.BEATHA ameongeza kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na halmashauri
mbili zilizopo wilayani Kibaha, kutatengwa maeneo maalum ya maegesho
ya bodaboda katika kurahisisha udhibiti wa chombo hicho cha usafiri na
kuondoa vurugu ambazo hazina ulazima.
Naye Mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda mjini Kibaham BW. ALLY
MAANDIKO amesema mpaka sasa chama chao kimeshaanda rasimu ya katiba
ambayo wanatarajia kuiwasilisha wizara ya mambo ya ndani kwa ajili ya
usajili wa kudumu.
BW. MAANDIKO amefafanua juu ya changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa
wanakabiliana zao ikiwa pamoja na baadhi ya watumishi wa serikali
kuingilia utendaji kazi wa chama hicho.
Afisa biashara wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BI. HAPPY CHINDULI
amesema mpaka sasa kwa upande wao zoezi la kutenga maeneo maalum kwa
ajili ya maegesho ya pikipiki linaendelea kwa lengo la kuboresha suala
zima la uchukuzi, na katika kusaidia kupunguza pengo la vijana wasio
na kazi katika halmashauri hiyo.
END
Comments
Post a Comment