SENSA-KIBAHA
SENSA YAENDELEA VIZURI KIBAHA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/28-08-2012
MKUU wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani Halima Kihemba amesema kuwa
zoezi la sense linaendelea vizuri pamoja na kuwepo kwa changamoto
kadhaa.
Akizingumza na waandioshi wa habari ofisini kwake, amebainisha kuwa
wananchi wameitikia vizuri hilo na kwamba wengi wamekubali
kujiandikisha tofauti na ilivyofikiliwa hapo awali.
Amesema kwamba kulikuwa na familia 25 korofi ambazo baada ya kupata
taarifa zake viongozi walizifikia na kuzipatia elimu juu ya umuhimu wa
sense na watu na makazi.
“Kati ya hao kaya 12 zilikubali kuhesabiwa na zilizobaki zinaendelea
kupatiwa elimu ili kuzishawishi kushiriki zoezi hilo linaloendelea kwa
siku saba,” alisema Kihemba.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi wilayani Kibaha mkoani hapa
limetupiwa lawama kwa kutowakamata wachochezi wanaolipinga zoezi la
sensa ili hali wakiwafahamu wanaosambaza nyaraka za uchochezi.
Taarifa kuhusu wachochezo hao zimeshafika kwenye ofisi ya Mkuu wa
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibaha (OCD) Francis Kibwengo (OCD) ambaye
ameonekana kuwa mzito kushughulikia suala hilo.
MWISHO.
Comments
Post a Comment