WATAKAOCHEZA NA SENSA KUFUNGWA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/24-Aug-12/05:05:14 PM Mkuu wa Mkoa wa Pwani, BI. MWANTUMU MAHIZA amesema wakati wa kubembelezana na kutoa elimu juu ya umuhimu mzima wa sensa ya watu na makazi umekwisha na kwa kubainisha kuwa suala hilo ni PRESIDENTIAL ORDER na yoyote atakaye vuruga zoezi hilo kwa sababu zozote atachukuliwa hatua stahili. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake maalum kwa jili ya sensa, BI. MAHIZA amesema utekelezaji mzuri wa zoezi hilo na kuweza kupata takwimu sahihi kutaiwezesha serikali kupanga mipango yake kwa ufanisi na kupunguiza kero kwa wananchi toka nchi imekuwa inakabiliana na mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Hivyo kwa mtu yoyote ambaye ana mpango wa kutaka kupotosha maana nzima ya Amri Jeshi Mkuu wa serikali kuhusina na zoezi hilo atakabiliwa na mkono wa sheria, na akasisistiza suala hilo siyo hiyari ni lazima kwa mtu yoyote ambaye atakuwa mtanzania, ambapo kwa Kibaha zoezi hilo litaenda sambmba na zoezi la utoaji wa vitambulisho vya Taifa na yoyote atakayekataa kushiriki zoezi hilo basi kuna uwezekano mkubwa wa kukosa kitambulisho cha Taifa. Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani, BI. MWANTUM MAHIZA ameelezea kushangazwa kwake na viongozi wa dini ambao wawashawishi waumini wao wagomee zoezi la sensa ya watu na makazi, kwa kuwaona wamekosa busara za kiuchamungu na wanajidhalilisha mbele ya jamii kwa kutotii mamlaka iliyopo duniani ambayo hata Mungu anaitambua, sasa iweje wajifanye wanampenda sana Mungu ambaye hawajawahi hata kumuona na kumchukia mwenzako uliye karibu naye, na ingekuwa vipi Mungu angekuwa tunamjua anakokaa. Amewasihi wananchi kuona fahari kuhesabiwa na kutambua mizizi ya utaifa wao, kwa wasipohesabiwa hapa kwenye asili yao wanategemea kuhesabiwa wapi, na kwa kufanya serikali hivyo itafaidika kwa kujua idadi ya wananchi wote wa Tanzania na kuiwezesha kupanga vyema mipango ya kimaendeleo na jinsi ya kugawa ziada ndogo ambayo inaipata kulingana na mahitaji. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA