YAMOTO BENDI KUWASHA MOTO MLANDIZI MEI MOSI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/29/2015 7:59:06 PM BENDI ya Yamoto inatarajiwa kutoa burudani kwenye mkesha wa siku ya wafanyakazi Duniani Mei Mosi Aprili 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa Container Bar Mlandizi wilayani Kibaha mkoani Pwani. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa baa hiyo Frank Mwalembwe alisema kuwa bendi hiyo katika kupamba burudani hiyo itasindikizwa na msanii wa kizazi Kipya Tunda Man ili kuwapa burudani wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani. Mwalembwe amesema kuwa lengo la kutoa burudani hiyo ni kuwaandaa wafanyakazi katika sherehe yao ambayo inafanyika kila mwaka ambapo kimkoa itafanyika wilayani Mafia. Amesema BW. MWALEMBE Burudani hiyo itakuwa ni nzuri kwa wakazi hao ambapo pia tutaishirikisha bendi ya JKT Ruvu kwa lengo la kutoa burudani hiyo ambayo itakuwa ya aina yake kwa wakazi wa Mji wa Mlandizi na vitongoji vyake na vile vya jirani. Amesema kuwa mbali ya wasanii hao pia kutakuwa na waimbaji chipukizi wa mkoa wa Pwani nao watapata fursa ya kuonyesha um...