NG'OMBE NI SHIDA BAGAMOYO-VIDEO
Ben Komba/Pwani-Tanzania/31 octoba 2014 Tatizo la unyanyasaji unaofanywa na wafugaji dhidi ya wakulima limefikia hatua mbaya baada ya wakulima kushindwa kufanya shughuli zao ambazo zilikuwa zinawapatia kipato. RFA ikiongea na BIBI.MARIAM ALLY Mkazi wa VIGWAZA amesema kuwa anasikitishwa na hatua ya mfugaji KINDETI kufungulia ng’ombe majira ya usiku na kuanza kura mazao yao, hali ambayo inawadhoofisha kiuchumi kwani anategemea kazi hiyo kujikimu na hali ngumu ya maisha. BIBI. MARIAM ALLY ameongeza kuwa mara zote wanapoenda kutoa taarifa katika uongozi wa kijiji, kunakuwa hakuna hatua yoyote inayochukuliwa kupambana na hali hiyo na hivyo kuwafanya wakulima kuwa na wakati mgumu kutafakari wataishi vipi baada ya mazao yao kuliwa na mifugo. Naye BI.HALIMA TILINDE amesema inapotokea kwenda kuripoti kwenye uongozi wanaambiwa kuwa wananchotakiwa kufanya ni kukamata mnyama husika na kumfikisha kituo cha Polisi, jambo ambalo limekuwa gumu kwa upande wao, kutokana na ku...