WAZAZI CCM WABEZA UKAWA

Ben Komba/Pwani-Tanzania

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa ndoa ya vya ma vya upinzini
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) si tishio kwani hizo
ni porojo tu na haitaweza kudumu.
Akizungumza kwenye baraza la mkoa la Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani
mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Jackson Josian alisema kuwa muungano huo
hautaweza kudumu.
Josian alisema kuwa hata wakiungana hawataweza kuisumbua CCM kutokana
na viongozi wao kutokuwa na ushirikiano kwani kila mmoja anaangalia
upande wake.
BW Josian.amesema Ndoa ya UKAWA haiwezi kudumu kutokana na wapinzani kuwa watu wa
vitisho tu na hawawezi kuongoza hata ndani ya vyama vyao,
Alisema kuwa kipimo kizuri kilikuwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba
ambapo walionyesha udhaifu mkubwa kwa kususia ambapo katiba ndiyo
mustakbali wan chi yoyote.ameongeza Wao wanaangalia maslahi ya vyama vyao na si maslahi ya Umma kwani
hata kama walikuwa na hoja za msingi wangepinga wakiwa ndani ya Bunge
na siyo nje hivyo hawa hawafai kupewa madaraka na ndoa yao haitutishi
kwani itavunjika
Kwa upande wake katibu wa CCM Kibaha Mjini Abdala Mdimu alisema kuwa
kipindi hichi ni vita kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa, Vijiji
na Vitongoji.
Mdimu alisema kuwa kwa sasa chama kiko kwenye mchakato wa kuwapata
wanachama wenye sifa watakaogombea nafasi za uenyekiti wa nafasi hiyo
ambapo kura za maoni zitafanyika Oktoba 30.
Aliwataka wanachama kutowachafua baadhi ya wagombea kwani mamlaka ya
kujua kuwa mgombea fulani hana sifa ni vikao ambavyo vikao vya
kisheria na si mtu kutoa maamuzi.
END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA