SHULE YAPATIWA VITABU VYA SAYANSI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/18-11-2014
Mkuu wa
wilaya ya Kibaha BIBI. HALIMA KIHEMBA amepokea msaada wa vitabu vya kufundishia
vya masomo ya Sayansi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kutoka
shule ya LATYMER ya Nchini Uingereza kwa shule ya sekondari ya Kata ya Mwambisi
katika suala zima la kukuza mshikamano kati ya shule hizo mbili.
BIBI.KIHEMBA
ameongeza kuwa msaada huo umekuja katika kipindi mwafaka wakati serikali ipo
katika vuguvugu la ujenzi wa maabara katika kila shule ya sekondari nchini kwa lengo la kuimarisha utoaji elimu katika
masomo ya sayansi.
Amesisitiza kuwa
ni jambo la muhimu kuzingatia usalama wa vitu ambvyo vimetolewa ili viweze
kuwasaidia na wengine ambao watabahatika kusoma shuleni hapo.
Aidha Mkuu
wa wilaya Kibaha BIBI.KIHEMBA ametoa ushauri kwa uongozi wa shule hiyo
kuanzisha na maabara ya kompyuta ili kupanua wigo wa utoaji elimu shuleni hapo.
Naye mwakilishi
kutoka BRITISH COUNCIL, BI.LILIAN MSUYA akikabidhi vifaa hivyo amesema wamekuwa
wakishirikiana na shule ya sekondari Mwambisi katika kuhakikisha Walimu
wanapatiwa mbinu bora za ufundishaji wa masomo ya Sayansi.
BI.MSUYA
amesema toka kuanzishwa kwa ushirikiana huo baadhi ya Walimu wameshatembelea
shule ya LATYMER ambayo ipo nchini Uingereza ili kwenda kujifunza kutoka kwa
wenzao.
Ameweka wazi
mafanikio ambayo wanategemea shule ya sekondari ya MWAMBISI kuyapata ni
pamoja na kujengewa uwezo na kuwa shule
ya mfano katika utoaji elimu mkoa wa Pwani.
END.
Comments
Post a Comment