UJENZI MAABARA WAPAMBA MOTO PWANI-VIDEO


Ben Komba/Pwani-Tanzania/12-11-2014
Katika utekelezaji wa agizo la Rais la ujenzi wa maabara kwa kila shule, Wananchi katika Kata ya Kongowe wamefanikiwa kupata vyumba vitatu vya maabar kupitia nguvu za wananchi na mchango kutoka mfuko wa Jimbo.

Diwani wa Kata ya Kongowe,BW.SLOUM BAGMESH amesema wao kwa upande wamejipanga toka mapema katika kuhakikisha wanatekeleza agizo la Rais la kutaka kila shule ya sekondari kuwa na maabara tatu ifikapo Desemba mwaka huu.

BW.BAGMESH ameongeza kuwa anamshukuru Mbunge wa Kibaha mjini, BW.SYLVESTRY KOKA kwa kuweza kutoa mabati 110 kwa ajili ya kuezekea shule ya Kata ya sekondari ya Mwambisi.

Amewataka wananchi kujitokeza kuchangia katika utekelezaji wa agizo hilo kwani hapo baadaye ni Taifa na jamii ambazo zitafaidika na maabara zetu, kwani zitawezesha kupatikana kwa wataalamu katika masuala ya sayansi na teknolojia.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Mwambisi, BW.JOSEPH SIMBA ameelezea kutiwa moyo kwake na juhudi mbalimbali zinazofanywa kuhakikisha maabara zinakamilika katika wakati ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza masomo ya Baiolojia, Kemia na Fizikia kwa kiwango stahili.

Naye mwenyekiti ya bodi ya shule, BW.SAID SHEKIUNGUE amesema kwa upande wao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani shule hiyo ilianzishwa mwaka 2013 ikiwa na darasa mmoja tu.
Lakini mpaka sasa shule hiyo ina madarasa takriban sita ambayo yanatumika kwa sasa na ilihali wakiendelea na ukamilishaji wa majengo hayo ya maabara.END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA