SUPER STAR YAJIANDAA NA LIGI YA MKOA DARAJA LA TATU-VIDEO


Ben Komba/Pwani-Tanzania/12-11-2014
Timu ya soka ya SUPER STAR ya wilayani Bagamoyo inayojiandaa na ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Pwani imeifunga Timu ya LUPUMOKO ya Kwamakocho kwa magoli 4-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Bongololo mjini Bagamoyo.

Mkurugenzi wa Timu hiyo ABDUL SHARRIF amesema wameanza kuiandaa timu hiyo takriban mwezi sasa, na lengo kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inapanda daraja na kuufanya mkoa wa Pwani hususan Bagamoyo inakuwa ina timu ambayo inacheza Ligi kuu na kwa sasa safari ndio imeshaanza.

Sharrif amebainisha katika kujiweka sawa ndio wakaona vyema kucheza na timu mbalimbali katika hali ya kujiweka sawa kwa ajili ya Mchezo kati yake na Timu ya Kombaini ya walimu kutoka Mkuranga Hapo Tarehe 16 novemba.

Naye kocha wa SUPER STAR, Mchezaji wa zamani wa timu ya Nyota Nyekundu na Simba katika nafasi ya golikipa, MTORO MAGOSO amesema timu yake imejiandaa vizuri na mechi inayoikabili ya ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa na hakuna hata mchezaji mmoja ambaye ana matatizo.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA