HARAKATI ZA KISIASA ZA PAMBAMOTO KIBAHA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania
Harakati za
kisiasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu zimepamba moto
kwa baadhi ya wanasiasa kujitokeza kutoka vyama mbalimbali kwa lengo la
kugombea nafasi za uongozi.
Mmoja wa
wanasiasa ambao nimekutana nae ambaye amenieleza kiu yake ya kugombea kiti cha
Ubunge kwa tiketi ya CCM, Ni Mwalimu mstaafu BW.ISRAEL SAZIA ambaye ni Pia ni
Mwenyekiti wa Kituo cha wasaidizi wa Kisheria mjini Kibaha.
BW.SAZIA
amesema amechukua uamuzi huo kutokana na uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika
masuala ya siasa na amepania kuwaletea maendeleo ya kweli wana Kibaha
akibahatika kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha
amewataka wapiga kura kujiepusha na watu wanaokuja Kibaha nyakati za uchaguzi
kwa lengo la kutaka kupata nafasi za kisiasa, ilihali wakiwa sio wakazi na
wenyeji wa Kibaha na hivyo kushindwa kuelewa kiini cha matatizo ya Kibaha.
Wakati
mgombea aliyejitokeza kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM anajinadi, Nao UKAWA
hawapo nyuma katika kuhakikisha wanatoa upinzania mkali kwa CCM ambapo
Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa CHADEMA,BW.FADHILI NGONYANI ameelezzea nia
yake ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa ya Machinjioni.
BW.NGONYANI
amesema wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya ukweli ya kimfumo nchini ili
kuwezesha kuharakisha harakati za kimaendeleo kwa jamii ya watanzania ambao kwa
sasa wanaishi katika umaskini mkubwa.
END.
Comments
Post a Comment