WAFUGAJI WALALAMIKA KUVAMIWA MAENEO YAO

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-11-2014

Wananchi wa kijiji cha wafugaji cha Mindu Tulieni kilichopo wilaya ya Bagamoyo wameitaka serikali kuwasaidia katika suala zima la wakulima kuvamia maeneo yao ilihali wakijua kuwa eneo hilo kuptia mpango wa matumizi bora ya ardhi limetengwa kwa ajili ya jamii ya wafugaji.

Mwandishi wa habari hizi akizungumza na MWmwenyekiti wa kijiji cha Mindu tulieni,BW. LETEMA SUNGUYA amebainisha kuwa imekuwa ni kawaida kwa wakazi kutoka maeneo ya Lugoba kuvamia maeneo tengefu ya wafugaji hali ambayo inasababisha uvunjifu wa amani hasa kipindi ambacho Ng”ombe kwa bahati mbaya akiiingia katika shamba la mkulima.

BW.SUNGUYA ameongeza kuwa suala zima la serikali kuleta mpango wa matumizi bora ya ardhi umelenga katika kujaribu kuepusha migogoro iliyokuwa inajitokeza mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima ambapo mara nyingi imesababisha vifo ambavyo vingeweza kuzuilika.

Naye Mwenyekiti wa kitongoji wa NADANYA,BW.ALOYCE PAUL ameelezea changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ya baadhi ya watu kuvamia eneo la ardhi yao ambayo imetengwa maalum kwa shughuli za ufugaji.

BW.PAUL amesema wakazi hao ambao wamekuwa mzigo kwa wakazi Mindu Tulieni kwani wamekuwa watu wasiojali suala zima la utunzaji wa mazingira, kutokana na wao kuuza maeneo yao kwa tamaa ya fedha na baadaye wanakwenda kufanya vurugu katika maeneo mengine na kwa makusudi kung"oa mawe ya mipaka kutimiza azma yao.

Hivyo Ni Wajibu Wa Serikali Kuzuia Viashiria Vya Uvunjifu Wa amani kwa kushughulikia matatizo katika hatua za awali na sio kujitokeza pale hali inapokuwa mbaya kama inavyoendelea hivi sasa wilayani Kiteto.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA