BILIONI 4 ZATOLEWA KWA AJILI YA MAABARA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/03-11-2014
Mkuu wa Mkoa
wa Pwani,BIBI.MWANTUMU MAHIZA amewataka watendaji katika halmashauri ya ya
wilaya ya Bagamoyo kulivalia njuga suala la ujenzi wa maabara ili kutekeleza
agizo la Rais JAKAYA KIKWETE.
Akizungumza
Katika Kikao Cha Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya
Bagamoyo,BIBI.MAHIZA amesema ni aibu kuona mpaka sasa hakuna maabara hata moja
ambayo imeshajengwa na akiuliza anawaambiwa ndio kwanza wanachimba msingi.
BIBI.MAHIZA
ameongeza kuwa kuanzia sasa madiwani wanatakiwa kubaki katika Kata zao ili
kusimamia ujenzi wa maabara za fizikia,Kemia na Bailojia ili kuweza kutekeleza
agizo la Rais.
Mkuu huyo wa
Mkoa wa Pwani BIBI.MAHIZA amefafanua kuwa halmashauri ya wilaya imebahatika
kupata mkopo wa shilingi bilioni 4 ambazo zimenuwiwa kwenda kujenga maabara mashuleni na kila kata
itawajibika kulipa shilingi Milioni 150 katika kata 22.
Aidha amemtaka
Mkurugenzi mpya wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, BW.IBRAHIM MATOVU
kuandika barua TRA ili kuiomba kuondoa ushuru wa vifaa vitakavyotumika kwa
ajili ya ujenzi wa maabara hizo.
NA katika
kulisimamia hilo Mkuu wa Mkoa wa Pwani ameweka kambi wilayani Bagamoyo ili
kuhimiza ujenzi wa maabara hizo na kila Mkuu wa Idara amepewa kata moja ya
kuisimamia na hasa ikizingatiwa kuwa suala la ujenzi wa maabara ni suala la
maendeleo.
END.
Comments
Post a Comment