BINTI APOTEA -VIDEO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania
Mtoto wa
kike BI.ELIZABETH SAMUEL mwenye umri wa miaka 13 mkazi wa Mailimoja shule amepotea
katika mazingira ya kutatanisha takriban wiki moja,mjini Kibaha mkoa wa Pwani.
Mjomba wa mtoto
ELIZABETH, BW.BONIFACE KITILA amesema siku aliyopotea alikuwa amevaa sketi ya
bluu ya shule na fulana ya rangi ya ugoro iliyokuwa na maandishi ya LOVE maeneo ya tumboni akiwa bila viatu.
Bw.KITILA
ameongeza kuwa mtoto huyo ambaye ni mgeni mjini Kibaha, ametokea Singida kwa
lengo la kuja kuishi na shangazi yake mjini Kibaha na mpaka sasa juhudi
mbalimbali zimeshafanyika ikiwa pamoja na kuripoti kituo cha Polisi.
Ametoa wito
kwa wananchi kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi watakapomuona mtoto
anayefanana na na wasifa uliotolewa,au apigiwe simu namba 0765871647.
END
Comments
Post a Comment